Sauti Sol waahidi utupu wao Arsenal ikishinda kisha.. wagwaya

 

 

Na Mwandishi wetu

Sauti Sol wamewatoa nishai wapenzi wao baada ya kushindwa kutekeleza ahadi ya kuwapa zawadi ya picha za uchi kama Arsenal itaichapa Chelsea 

Katika majibizano na wapenzi wao katika mtandao wakali hao walisema kwamba  Arsenal ikimtandika Chelsea basi watapiga picha za utupui na kuziposti.

Katika kipute kilichopigwa Derby  Jumapili, Arsenal iliichapa Chelsea 2-0  na kuwaacha wapenzi wa Sauti Sol wakisubiri zawadi yao ambayo hadi leo haijatolewa.

Wanamuziki hao ambao walisema kila mmoja atatoka kama alivyoletwa duniani, walishindwa na kulaumu teknolojia kwa kusababisha wasiposti walichowaahidi wapenzi wao.

Hata hivyo wapenzi wao wamesema kwamba kushutumu keyboard haikuwa halali kwani walifanya uhariri katika Instagram na Facebook lakini kwenye Twitter  walisema kuna shida katika autocorrect.

Mmoja wa wanamuziki Savara Mudigi yeye aliweka nusu zawadi kw akuposti picha ya kifua wazi, lakini wadada waliochangia katika picha hiyo walimdai atoke wote kama alivyozaliwa.

Januari 19 katika posti yao ya twita  Sauti Sol walisema n*des kama Arsenal watashinda lakini wakisubiri baada ya gemu Sauti Sol walisema Aito correct imefanya mambo ambayo wao hawakuyatamka.

“Guys, guys, guys!. This autocorrect is a b*tch. So stop camping here waiting for weird things,” waliandika.

 Sauti Sol naked