“Ni na ndoto ya kupeleka muziki wangu nchi zaidi ya 50”- mwimbaji chipukizi Winnie Mbilingi

 

*Anatamba na wimbo wa u mwema

*Anatarajia kuzindua albam yake mwakani

 

Winnie Mbilingi

Winnie Mbilingi

Na Mwandishi wetu,

Mwimbaji chipukizi Winnie Mbilingi kutoka Tanzania, amesema ana maono makubwa, ya kutoa album mwaka huu, ambayao itamplekeka  zaidi ya nchi 50.

Winnie alianza safari yake ya uimbaji nyimbo za injili rasmi mwaka jana tu, anatamba na wimbo wa U Mwema, unaofanya visuri nchini Tanzania.

“Ni na ndoto ya kupeleka muziki wangu nchi zaidi ya 50!” alisema hivi karibuni akizungumza na faidabook.com kuhusu safari yake ya uimbaji.  Anaamini Mungu atamusaidia, kukamilisha ndoto yake.

Winnie Mbilingi alisema kuwa ukosefu wa fedha ni moja ya changamoto inasababisha  watu wengi kushindwa kufikia malengo yao ikiwemo waimbaji kushindwa kukamilisha kazi zao kwa wakati .

“Nilishindwa kukamilisha wimbo wangu wa kwanza unaoitwa u mwema kwasababu nilikuwa sina fedha ya kulipa na niliwaomba  kunirekodia wimbo kwa mkopo ambapo walikubali kunikarekodi wimbo huo mwaka 2017. Mwaka 2018 nilifanikiwa kupata fedha nikalipia,”alisema Winnie.

Winnie ambaye amesomea fani ya uhasibu anatamba na wimbo wa u mwema  anasema alianza kuimba akiwa mdogo kisha akajiunga na kwaya ya kanisa la KKKT  Chunya nyikani kwaya 2009 na yuko katika maandalizi ya kutengeneza video ya wimbo huo inayotarajiwa kukamilika mwaka hu una pia atakamilisha wimbo wake wa pili hivi karibuni unaoitwa Inuka.

“Nimekamilisha nyimbo mbili za audio na natarajia kutengeza video yangu ya wimbo wa u mwema mwaka huu “

Alisema wakiwa Shule ya Sekondari Mpanda Girls walibahatika kuwa na kikundi kilichoitwa Glory kilichoundwa  na wasichana wanne ambao ni huruma mwanda, rose kafyanya na happy makazi na kilifanya vizuri baadaye walitengana walipomaliza shule ndipo akaanza kuimba mwenyewe.

 

Aidha amewataka waimbaji wengi kutokata tamaa katika safari yao ya uimbaji   na kuwa waaminifu huku wakiamini kuwa wanaweza kufanikiwa kwa wakati kadiri Mungu anavyopenda.