Staa anyimwa ruhusa ya kufanya mapenzi

Mike Sorrentino

Mike Sorrentino

Mike Sorrentino hakutarajia alichoambiwa na wakuu wa jela kwamba hataona undani wa mkewe kwa miezi 8 zaidi ya kupigwa kisi wakati atakapokuwa jela.

Ameambiwa na wahusika kwamba muda wote atakaokuwa ameketi huko jela hatapewa faragha ya aina yoyote ile wakati mkewe atakapofika hapo ikimaananisha kwamba hawawezi kungonoana na mke wake huyo ambaye wamefunga ndoa hivi karibuni.

Mume huyo mpya ambaye amejijengea umaarufu katika ‘Jersey Shore’ ametupwa jela kwa miezi 9 kwa kukwepa kodi.

Mike “The Situation” Sorrentino na mkewe Lauren Pesche (33) hawataweza kuonana kimwili wakati jamaa akiwa gerezani kutokana na agizo lililotolewa kwamba hana ruksa ya kupata safari za kimapenzi zenye uhalisia kutoka kwa mkewe.

Kijana huyo wa miaka 36 anayetamba sana kwenye kipindi cha televisheni cha Jersey Shore anatumikia gereza la Otisville lililopo jijini New York.

Mike amepewa nafasi ya kuonwa na mkewe mara moja kwa wiki na ataruhusuwa kupigwa kisi ya salamu na ya kuagana tu na wala hatapewa nafasi ya faragha.

Dan Wise, Msemaji wa gereza hilo amesema kwamba anachoweza kufanya muda wote atakapokuwa gereza ni kufanya mapenzi ya simu au kuandikiana barua ne mkewe, kitu ambacho wafungwa wengi wanakifanya kupata nafuu.

Mike atatumikia miezi minane jela na akitoka atakuwa na saa 500 za kujitolea ambazo ni sawa na miaka miwili .

Alihukumiwa kutupwa jela Novemba Mosi mwaka jana baada ya kupatikana na hatia ya kukwepa kodi.Ametakiwa kulipa dola za Marekani 123,913 na tayari ameshalipa.

 

Kwa kushindwa kufanya mapenzi jamaa akiwa ametupwa jela kumeelezwa kuwa ni pigo kwamba kwa wanandoa hao ambao wanajinadi kama marafiki wazuri sana ambao kila kitu wanaweza kusaidiana kuweka sawa maisha yao.