UCHAMBUZI WA TWEETS Shindano la Reginald Mengi

UCHAMBUZI umefanywa na Dr Donath R.Olomi. Director of Institute of
Management and Entrepreneurship Development (IMED)

Mwezi Juni tulipata jumla ya tweets 1510!.

Yametolewa mawazo mengi juu ya namna ya kuondoa umaskini ambayo
yamegawanyika katika sehemu tatu:

1) Jinsi mtu binafsi anaweza kufikiri na kutenda ili asiwe maskini au
aondoke kwenye umaskini
2) Jinsi jamii inavyotakiwa kufikiri na kufanya kuondoa umaskini
3) Nini kinachotakiwa kufanywa na serikali au wadau wengine kuondoa watu
kwenye umaskini

Kama nilivyoahidi, nimechagua tweet moja iliyonigusa kuliko zote kupata
zawadi ya kwanza ya shilingi milioni 1.

Katika kufanya uchaguzi, nimeangaliza vigezo vitatu muhimu:

1) Wazo linaloeleweka na kuelezeka kirahisi
2) Wazo bunifu – lisiwe jambo ambalo nimelisikia au kuliona kwenye sera
au mipango ya nchi, au lisiwe ni msemo ambalo nimeshausikia au kuuona
3) Wazo linawezekana kutekelezwa katika mazingira ya Tanzania
Mawazo mengi yalielekea kufanana kwa ubora, hivyo ilikuwa vigumu kufanya
uchaguzi.