Press Release Tanzania Forest Services Agency (Kiswahili)

MKAKATI WA KUDHIBITI BIASHARA YA MAZAO YA MISITU KINYUME CHA SHERIA PAMOJA NA KUBORESHA UKUSANYAJI MADUHULI

1. UTANGULIZI
Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (Tanzania Forest Services Agency) –TFS- umeanzishwa kwa kuzingatia Sheria ya Wakala wa Serikali Namba 30 ya 1997 iliyorejewa 2009). TFS ilianza kazi rasmi Julai 1, 2011 ikiwa na lengo la kutekeleza majukumu ya kiutendaji ya uhifadhi na usimamizi wa rasimali za misitu na nyuki kwa ufanisi na tija zaidi.
Wakala unatakiwa kuendesha shughuli za uhifadhi na usimamizi wa rasimali za misitu na nyuki kwa kujitegemea kwa asilimia 100 pamoja na kuchangia fedha katika mfuko mkuu wa Serikali yaani Hazina. Ili kufikia azma hii Wakala unajizatiti katika kudhiti biashara haramu ya mazao ya misitu inayofanywa kinyume cha sheria na kuboresha ukusanyaji wa maduhuli, kubaini mianya iliyopo ya ukwepaji kulipa ushuru wa mazao ya misitu na kutafuta mikakati ya kuidhibiti.
2. HATUA TULIZOCHUKUA
Wakala umefanya ukaguzi maalum wa namna biashara ya mazao ya misitu na ukusanyaji maduhuli inavyosimamiwa katika maeneo mbalimbali ili kubaini na kujionea hali halisi katika kudhibiti biashara ya mazao ya misitu na kukusanya maduhuli kwa nchi nzima kuanzia tarehe 7/05 – 21/05/2012. Katika ukaguzi huo makundi 11 yalifanya kazi katika maeneo mbalimbali kwa lengo la kuboresha ukusanyaji maduhuli, kuimarisha makusanyo na kupunguza kasi ya uharibifu wa misitu nchini. Ukaguzi na uhakiki wa nyaraka ulifanyika katika Ofisi za Maafisa Misitu Wilaya, Maafisa wa Vituo vya Ukaguzi, maeneo ya uvunaji na kwa wafanyabiashara ili kuangalia kama taratibu, kanuni na sheria dhidi ya kumiliki na kusafirisha mazao ya misitu zinazingatiwa. Kazi hii ilifanyika usiku na mchana.Ukaguzi umeokoa fedha ambazo zilipaswa kukusanywa kama maduhuli ya Serikali pamoja na kukamata mazao yalivyovunwa au kumilikiwa kinyume cha sheria pamoja na ada za makampuni ya uchimbaji madini na minara ya simu. Katika zoezi hili jumla ya Shilingi 744,340,146/= zilikusanywa. Hali kadhalika tuliweza kukamata mazao ya misitu kama mkaa, mbao na magogo yaliyovunwa kinyume cha sheria yenye thamani ya Shilingi 33,068,390/=. Jumla Shilingi 777,408,536/= fedha taslim na thamani ya mazao ya misitu yaliyokamatwa. Vile vile, kuna fedha shilingi 35,485,000/= ambazo zinatakiwa kulipwa kama ada za kampuni za uchimbaji madini na minara ya simu. Katika kipindi cha mwaka huu wa fedha hadi Mei 2012, Wakala umefanikiwa kukusanya Jumla ya Shilingi 59,328,190,572.26 ambazo ni sawa na asilimia 110 ya lengo la mwaka huu wa fedha.
3. CHANGAMOTO
3.1 MAMBO TULIYOJIFUNZATathmini ya zoezi hili imefanyika na kutuonyesha changamoto zinazotukabili katika maeneo yafuatayo:- (i) Usimamizi wa rasilimali za misitu(ii) Mfumo wa Utendaji(iii) Watumishi na Vitendea Kazi mfano Usafiri na Nyaraka
3.2 MIKAKATI YA KUKABILI CHANGAMOTO
a) Kuimarisha uhifadhi na udhibiti wa Misitu ya Hifadhi ya Asili pamoja na biashara ya Mkaa na Mbao
i) Kutoa elimu kuhusu usajili, wajibu na majukumu ya wakala, taratibu za kufanya biashara ya mazao ya misitu, kukumbushana malengo na mafanikio yaliyofikiwa na TFS ii) Kufanya utambuzi wa Misitu – mipaka kubainishwa iii) Kudhibiti uvunaji katika Wilaya ambazo hazina mpango ya uvunajiiv) Kuweka Maafisa Leseni za msitu katika maeneo muhimuv) Kuwa na vitabu vya regista za wateja, na wilaya kupata orodha halisi ya wafanyabiashara waliosajiliwavi) Kuanzisha stock register ya wateja itakayorahisisha ukaguzivii) Kuanzisha bustani za upandaji mitiviii) Kuimarishe Vizuia vya mipakani ili kuhakikisha mazao yanakotoka, kuwa na nyundo maalum kwa ajili ya mazao yanayotoka nje ya nchi ix) Kuhakikisha taratibu za ushuru wa madini zinasimamiwa ili kuongeza udhibiti
b) Kuimarisha Mifumo ya ukusanyaji
Kuwa na hatua za utekelezaji katika udhibiti kama ifuatavyo:(i) Kuhakikisha biashara za mkaa na mbao zinadhibitiwa: • Kuhusu mkaa, ushuru uzingatie uzito na uvunaji ufanyike kwenye maeneo yaliyoainishwa pamoja udhibiti katika idadi ya magunia yanayozidi• Mbao/ Magogo yalipiwa kufuatana na ujazo halisi(ii) Kuhakikisha elimu ya maadili inatolewa kwa watumishi na wafanyabiashara wanaelimishwe kuhusu taratibu za biashara kwa kufuata kanuni na sheria. Pia tutatoa hamasa na elimu ya teknolojia mbadala ya utengenezaji wa mkaa na kutumia majiko banifu (iii) Kuwa na vituo vya ukusanyaji wa mkaa (iv) Kuhakikisha Wafanyabiashara wa mazao ya misitu wanaunda vyama vyao;(v) Kudhibiti idadi ya mazao ya misitu yanayosafirishwa kwa kuwa na jedwali la mahesabu c) Kuwapatia motisha na vitendea kazi kwa watumishi (i) Kuhakikisha kuwa TFS kwa kushirikiana na Halmashauri za wilaya zinakuwa na watumishi wake katika maeneo muhimu mfano Rufiji, Kilwa, Liwale, Masasi, Ruangwa, Nachingwea, Tandahimba, Mtambawala na Nanyumbu(ii) Kuongeza watumishi kwenye vituo vya udhibiti (Kisosi na vizuia) vyenye upungufu (iii) Kujenga ushirikiano na mahusiano mazuri kati ya watendaji wa vizuia, vikosi na halmashauri (iv) Kutoa motisha kwa watumishi pale wanapofanya masaa ya ziada au kazi nzuri na kuwachukulia hatua za kisheria pale wanapokiuka sheria(v) Kutoa elimu zaidi kuhusu sheria, taratibu, miongozo na kanuni, elimu hiyo itolewe kwa vitendo (practical training) (vi) Kuhakikisha nyaraka zote za makusanyo zinapatikana kwa wakati vituoni(vii) Kupeleka vitendea kazi kama pikipiki kwenye maeneo muhimu (viii) Kuhakikisha TFS inakuwa na waendesha mashitaka wake, watu wenye nia na uwezo watabainishwa na kupelekwa kwenye semina maalum kwa ajili ya kazi hiyo.

4 HITIMISHO
Kufuatana na ukusanyaji maduhuli pamoja na mikakati ambayo tumeianzisha napenda kuwaambia kwamba tutahakikisha tunaendeleza mikakati hiyo na kuifanya kuwa ya kudumu na siyo ya mptio na kwamba taarifa mbalimbali zitaendelea kutolewa kuhusu maendeleo ya utendaji wa wakala kila itakapobidi.
Juma S. MgooMtendaji Mkuu Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania