MSONGAMANO WA NDEGE WAPUNGUA BAADA YA UKARABATI- NDEGE 30 ZATUA KWA SAA BADALA YA 8

]

SERIKALI imesema kwamba msongamano wa ndege zinazosubiri kutua au kuruka
katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere umepungua baada
ya kufanyika kwa ukarabati mkubwa ambao umeongeza uwezo wa kuhudumia ndege
30 kwa saa badala ya nane.

** **

Kauli hiyo ilitolewa leo (jana) na Waziri wa Uchukuzi, Omari Nundu katika
sherehe ya kuadhimisha siku ya kimataifa ya usafiri wa anga duniani
zilizofanyika kwenye viwanja vya Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania(TAA)
jijini Dares Salaam.

** **

Ambapo kauli mbiu yake ni ‘Kusaidiana na Kushirikiana kwa ajili ya Usafiri
Endelevu wa Anga Duniani’.

** **

“Wizara kupitia Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania imekamilisha
matengenezo makubwa ya miundombinu na uboreshaji wa mitambo… Mategenezo
haya yamejumuisha ukarabati mkubwa wa njia ya kurukia ndege, viungio vyake
na maegesho ya ndege,”alisema Waziri Nundu.

** **

Waziri Nundu aliongeza kuwa serikali itaendeleza juhudi za kuboresha
miundombinu na ubora wa huduma za usafiri wa anga katika viwanja vya ndege
nchini hadi viwepo vya kutosha vya kuweza kuhudumia nchi nzima. Hivyo kwa
kuanzia serikali imepanga kushughulikia viwanja 17.

** **

Aliongeza kuwa ili usafiri huo uwe endelevu,uwepo wa wataalam wa usafiri wa
anga ni muhimu. Serikali itashirikiana na mamlaka hiyo na wadau wengine
kuhakikisha kuwa Watanzania wengi wanapata mafunzo hayo.

** **

Aidha Waziri Nundu alisema hatua za haraka zinapaswa kuchukuliwa katika
suala hilo kwa kuwa marubani na wahandisi wengi wazalendo wana umri wa
miaka zaidi ya 50, ambapo aliishauri mamlaka hiyo na wadau kuanza taratibu
za kuimarisha mfuko wa mafunzo huku akiutaka uwe endelevu.

** **

Naye Mkurugenzi Mkuu wa mamlaka hiyo, Fadhili Manongi alisema idadi ya
abiria wanaotumia usafiri huo imeongezeka kutoka 1,206,821 mwaka 2000, hadi
abiria 3,027,512 mwaka 2010 ambapo ni sawa na ongezeko la asilimia 151.

** **

Alisema safari za ndege pia zimeongezeka kutoka 112,821 hadi 181,240 katika
kipindi hicho kwa asilimia 61 na kuhusu utalii nchi ilipokea 782,699 kwa
mwaka 2010 ukilinganisha na watalii 501,669 mwaka 2000.

** **

Manongi aliongeza kuwa asilimia 50 au 60 ya watalii hutumia usafirihuo na
iliyobakia wa barabara hawa wanaotoka nchini Kenya baada ya kuwasili kwa
ndege nchini humo.

Mwisho.

** **

** **