MATUMLA, MIYAYUSHO WAPIMA UZITO LEO KWA AJILI YA MPAMBANO KESHO

Dar es Salam:
Mabondia Mbwana Matumla ‘Golden Boy’ na Francis Miyayusho ‘Chichi
Mawe’ leo wamepima uzito kwa ajili ya mpambano wao wa Ubingwa
utakaofanyika katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es salaam kesho
jumapili OKCTOBA 30.

wakizungumza wachezaji hawo kwa wakati tofauti baada ya kupima
wamesema wapo tayari kuonesha mchezo mzuri wa ngumi na kuwapa raha
zisizo na kifani kwa sababu akuna kisingizio chochote kile kwa kua
tumejiandaa vya kutosha

Licha ya mabondia hawo kupima uzito pia wamepima vipimo mbalimbali
ususani Ukimwi, Mkojo kwa ajili ya kuangalia kama mabondia hao kama
wanatumia madawa ya kuongeza nguvu.

Pambano hilo kubwa litakuwa la 12 la uzito wa Bantam, ambapo kabla ya
mpambano kutakua na mapambano mengine ya utangulizi.

Mapambano hayo ya kati ya Juma Fundi na Fadshili Majia, Mohamed
Matumla na Ramadhani Mashudu, Issa Sewe atazidunda na Ramadhani Shauli
wakati kwa upande wa ngumi za wanawake Asha Nzowa (Asha Ngedere)
atazichapa na Salma Kihobwa (mwajuma Ndalandefu)

Katika Mchezo huo kutakua na DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja
na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha
wa mchezo huo Rajabu Mhamila ‘Super D Boxing Coach’ kwa ajili ya
kuwapa mambondia mbalimbali mbinbu za mchezo na mashabiki kujua sheria
za masumbwi.

Super D alisema katika DVD hizo kutakuwa na mapambano mengi ambayo
yanaweza kutumika kama mafunzo muhimu kwa mabondia ,makocha marefa
pamoja na mashabiki wa mchezo kujua sheria mbalimbali.

” Kuna mapambano kama ya akina Amir Khan, Manny Paquaio, Floyd
Maywhether, David Haye, MOhamedi Ali pamoja na mtanzania Roja mtagwa
anaefanya shughuli zake Marekani,

DVD hizo ni nzuri na hata walio tayari tayali katika mchezo huo
wanatakiwa kujua sheria na mafunzo ya ngumi mana zinafundisha mambo
mengi ” alisema Super D;