*TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI KUTOKA FEMACT: *
*
*
Sisi Muungano wa Asasi za Kiraia zinazotetea Usawa wa jinsia, haki za
binadamu, demokrasia na ukombozi wa wanawake kimapinduzi (FemAct) tumepokea
kwa mshtuko, mshangao na masikitiko makubwa, tuhuma kuwa Katibu Mkuu,
Wizara ya Madini na Nishati, ameandaa mpango mahususi wa kukusanya pesa
kutoka idara na wakala walio chini ya wizara yake, kwa ajili ya kuhonga
Wabunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ili wapitishe bajeti ya wizara
hiyo.****
Kwetu sisi wanaharakati, kitendo hiki ni ishara ya mambo makubwa zaidi
yanayofanywa na baadhi ya viongozi wetu yanayosababisha kuendeleza ufukara
na umaskini wa taifa letu na watu wake.****
Kama tuhuma hizi ni za kweli, ni wazi kuwa mikakati mingine kama huu
haikuanza mwaka huu, na hauwezi kuwa mkakati wa Wizara ya Madini na Nishati
pekee. Na kama hivyo ndivyo, basi Serikali ya Tanzania yote inanuka rushwa,
na haina uhalali wa kuendelea kuongoza nchi, Serikali na Watanzania.****
Hali hii inatufanya tuzidi kuamini kuwa Serikali inayoghubikwa na
kuendeshwa kwa mfumo wa kuhongana miongoni mwa viongozi na watendaji wenye
mamlaka ya kufanya maamuzi katika mihimili mikuu ya dola, ni Serikali ya
hatari na isiyostahili kuendelea kuwa madarakani. Serikali ya namna hii
haiwezi kuwa na utashi wa kutumikia matakwa ya wananchi, isipokuwa
kununuliwa na mafisadi.****
Uchambuzi yakinifu wa bajeti tunaofanya mara kwa mara sisi wanaharakati
unatuonesha jinsi gani rasilimali za taifa hili zinavyoendelea kufaidisha
wachache na kudumisha ufukara kwa wengi. Wanaharakati wa FemAct tunasema
kwamba tatizo hili ni kubwa na lisiishie tu kwenye kuwaadhibu waliyohusika
na rushwa ya kupitisha bajeti. Tatizo ni pana zaidi na linahitaji tafakari
pana ya kimfumo.****
*Tatizo la Umeme*
Tatizo la umeme sio la leo, ni suala ambalo limekuwa likipigiwa kelele kwa
muda mrefu, Serikali imekosa mbinu na mikakati sahihi hadi kufikia hatua ya
kutaka kubinafsisha Shirika la Ugavi wa Umeme (Tanesco). Mikataba mingi
michafu imeingiwa na Serikali kwa kutumia makampuni makubwa ya nje kama
IPTL, Agreco, Songas, Richmond, Dowans na NetGroup Solutions. Hakika mbinu
chafu zisingezaa matunda mema; tatizo la kukosa umeme limeongezeka mara dufu
na wakati wote huu mwananchi masikini anaendelea kuteseka licha ya kulipia
gharama zote anazobebeshwa na viongozi waongo na wanaokubali kuhongwa.****
Lakini katika mazingira haya ya rushwa, utapeli na ufisadi, Serikali imekosa
utashi wa kushughulikia tatizo la umeme kwa kuzingatia mipango ya muda mrefu
kama Miradi ya Makaa ya Mawe, Mchuchuma , Ngaka na Kiwira, ambavyo kwa
pamoja ina uwezo wa kuzalisha megawati 1500 za nishati ya umeme ambayo
inatosha kumaliza tatizo lililopo kwa takribani miaka mingi ijayo.****
Inashangaza kuona taifa lenye rasilimali nyingi na miaka 50 baada ya uhuru
likizalisha megawati 1034, wakati vyanzo vitatu vilivyotajwa hapo juu
vingezalisha megawati 1500.****
Mbali na mradi wa Mchuchuma, maporomoko ya mto Rufiji ya Stgiler’s Gorge,
yana uwezo wa kuzalisha megawati zaidi ya 2,000 za umeme wa gharama nafuu.
Lakini kila mwaka tunasikia ahadi kuwa mradi huu utaanza bila mafanikio
matokeo yake tumeendelea kung’ang’ania kukodisha majenereta kutoka Ulaya na
Marekani ambayo baada ya muda mfupi hushindwa kufanya kazi wakati mwingine
kutuingiza kwenye mikataba michafu ya kifisadi.****
*Umeme kwa ajili ya nani?*
FemAct tunataka kuona umeme ukiwa ni nishati muhimu kwa kila raia wa taifa
hili, masikini wa kijijini na wa mjini, unaopatikana na kwa bei ambayo
inaruhusu kila mwananchi anaweza kumudu gharama zake.****
Ingawaje Tanzania ina utajiri mkubwa wa vyanzo vya nishati kama vile
gesimoto(geothermal) nishati ya jua na upepo, pamoja na mkaa wa mawe,
takribani
asili mia 39% ya wakazi wa mijini na asili mia 2% tu ya wakazi wa vijijini
wenye kufikiwa na umeme. Asilimia 10 ya kaya zote ndizo zinapata umeme kwa
kupitia gridi ya taifa, na 1% tu ya kaya zote za Tanzania zinauwezo wa
kutumia umeme kwa ajili ya kupikia. Wakati tukidai kwamba taifa limekumbwa
na dharura kuwa gizani takribani nusu mwaka sasa, asili mia kubwa ya
watanzania wako kwenye hali hii ya hatari takribani miaka hamsini tangia
tupate uhuru. ****
Iweje, miaka hamsini tangu tupate uhuru Taifa liko gizani? Iweje wazalishaji
wakuu wa chakula, mazao ya biashara na walezi wa watoto wa taifa hili wawe
kwenye giza kuu tangu bendera ya mkoloni kushushwa na kupandishwa kwa
bendera ya Taifa huru? Iweje asili mia sabini hadi tisini ya Watanzania
wamekuwa wakitegema aidha mkaa au kuni kwa ajili ya kupata nishati ya
matumizi ya kaya? Matokeo yake yameendelea kuwa mzigo mkubwa wa wanawake
wazee kutafuta na kubeba kuni, kupikia kwa kutumia kinyesi cha ng’ombe huku
wakikumbana na vitendo vya ukatili wa kijinsia kutokana na macho yao kuwa
mekundu.****
*Kwanini serikali itoe rushwa?*
FemAct inaamini kuwa kuna sababu nyingine inayolazimisha Serikali kujaribu
kutoa rushwa ili kupitisha bajeti ya Wizara ya Madini na Nishati ni mfumo
mzima wa mikataba, uwekezaji, usimamizi na uendeshaji wa shughuli za madini
na gesi asilia hapa nchini ambao hauna uwajibikaji; na uwazi wake una
mashaka na hivyo kuhalalisha vitendo vya rushwa na ufisadi. Watanzania
hawanufaiki na madini na gesi asilia kutoka nchini mwao. Kuna migogoro
mingi katika maeneo yanakochimbwa madini na gesi asilia baada ya wananchi
kugundua ulaghai unaofanywa na baadhi ya watendaji wa serikali kwa
kushirikiana na wawekezaji katika migodi ya madini na visima vya gesi
asilia.**
Kutokana na masuala yaliyoorodheshwa hapo juu, FemAct inataka Serikali
ifanye marekebisho haraka kukidhi haja ya madai yafuatayo:-****
1. Katibu Mkuu,Waziri ,Naibu wake kwa pamoja na watendaji wengine
waliohusika kuchangisha fedha za kuwahonga wabunge waondolewe kazini na
kuchukuliwa hatua za kinidhamu na kisheria haraka. Matendo yao ni kinyume
na Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Namba 11 ya mwaka 2007.****
2. Tunamtaka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania awafute kazi
watendaji hao mara moja na kuwachukulia hatua za kisheria ili iwe mfano kwa
wahalifu wengine waliojificha katika ajira za Serikali.****
3. Katika marekebisho ya bajeti ya Wizara ya Madini na Nishati Serikali
ilete mikakati sahihi ya kulimaliza tatizo la umeme nchini. Serikali itaje
vyanzo mbadala vya kuaminika vya kuzalisha umeme na sio kukodisha majenereta
na kujiingiza kwenye mikataba ya kifisadi.****
4. Serikali ieleze hatua thabiti inazozichukua kuhakikisha vyanzo vya
umeme wa upepo, nguvu ya jua,makaa ya mawe,maporomoko ya mto Rufiji,
yanatumika ipasavyo kuzalisha umeme badala ya kuingia mikataba na makampuni
ya kitapeli na kutegemea umeme wa mvua.****
5. Kamati ya kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ieleze sababu za
kushindwa kugundua mapungufu katika bajeti hiyo mapema na kuirudisha
serikalini badala ya kupoteza muda wa umma.****
6. Serikali ielekeze nguvu ya kufikisha umeme kwa wananchi wa vijijini na
kwa bei rahisi ili kuongeza tija katika uzalishaji hasa kupitia kilimo na
kuongeza ari ya kuanizishwa kwa viwanda vya kusindika mazao vijijini.***
*
7. Serikali iwe wazi katika shughuli zake zote, hususan, mikataba ya
madini, kufua umeme na kuzidua gesi asilia.****
8. Serikali iunde tume huru kuchunguza mauaji ya hivi karibuni huko
Nyamongo Mara na hii itamkwe ndani ya bajeti kwamba serikali itawalinda
wananchi wake waishio jirani na migodi kwa mali zao na usalama wao. Vile
vile serikali itoe tamko hatima ya mgodi wa Buhemba.****
9. Serikali iweke wazi mikataba yote ya madini iliyopo ili kutoa fursa
kwa umma kudadisi ikiwa ina maslahi kwa taifa. Zoezi la kuweka mikataba yote
ya madini hadharani ni muhimu sana kuliko kuendelea kuvutia wawekezaji wapya
katika sekta za nishati na madini ambazo zimeghubikwa na kashfa za ufisadi
na uzembe.****
*Imetolewa Dar es salaam na*:****
…………………………….**
*Usu Mallya*
*Kny Sekretarieti ya Femact*