Watanzania Wajizatiti Twitter

by Chambi Chachage:

Watanzania wanazidi kujumuika katika Twitter kujadili masuala mbalimbali!
Mijadala hiyo ina mvuto sana hasa ukizingatia kuwa viongozi wa
kijamii, kibiashara na hata kisiasa wanajumuika. Wapo Wabunge (mf.
@DocFaustine na @zittokabwe), Wakurugenzi wa Makampuni (mf. @iMashibe
na @beyakuze), Wanazuoni (mf. @Mwanasosholojia na @Mwanafalsafa) ,
Wanamuziki (mf. @mwasitiJ na @Profesa_Jay), Waandishi wa Habari (mf.
@kabsjourno na @salvarweyemamu), Watangazaji (mf. @barbarahassan na
@nyangorojs)Wanaharakati (mf. @Irenei2011 na @rakeshrajani), Asasi za
Kiraia (mf. @Darajatz na @HakiElimu) Mawaziri (mf. @AnnaTibaijuka na
@Mnyambi ) – na hata Rais wa Nchi na Mama wa Kwanza (@jmkikwete na
@salmakikwete)!
Kwa sasa mijadala mikali inayoendelea ni pamoja na wa #udinitz na
#mashoga. Jana kulikuwa na mjadala mkali sana kuhusu #DowansAward
ambao bado unaendelea. Hivi karibuni pia kulikuwa na mjadala mkali
kuhusu ajali ya meli Zanzibar #ZanzibarBoatAccident . Udadisi
ilijiunga rasmi mwaka jana baada ya kusitasita kwa muda mrefu (rejea
http://udadisi.blogspot.com/2010/12/twittering-tanzanias-transinformation.html)