*TAARIFA KWA UMMA*
*MAELEZO KUHUSU MAKALA ILIYOTOLEWA NA GAZETI LA MWANANCHI KUHUSU UBOVU WA
MAJENGO UDOM TAREHE 12 AGOSTI 2011*
Gazeti la Mwananchi la tarehe 12 Agosti 2011 ukurasa wa 8 liliandika makala
kuhusu Chuo Kikuu cha Dodoma yenye kichwa cha habari:*Ubovu wa Majengo UDOM;
tatizo linalohitaji kumulikwa haraka *na mwandishi Habel Chidawali.****
Katika makala hii kuna mambo ambayo hayakuwekwa sawa na mwandishi.Chuo
kinapenda kuyaweka sawa ifuatavyo;****
1.Mwandishi ameeleza kuwa uongozi wa Chuo unaficha habari na hasa zile
zinazoonekana kukosoa.Jambo hili tunalikanusha kwa dhati kwani Makamu Mkuu
wa Chuo amekuwa mstari wa mbele katika kuwapa habari waandishi na pia
amekuwa akiwasisitiza kuwasiliana nae muda wowote wanapotaka kujua jambo
lolote.Sio hivyo tu bali amewapatia waandishi fursa ya kutembelea majengo
ya Chuo wakati wowote ili kujiridhisha. ****
2.Suala la ubovu wa majengo ambalo mwandishi alieleza kwamba majengo
yanavuja.Chuo Kikuu cha Dodoma kina vyuo sita na tayari vyuo vinne vina
majengo yake.Mwandishi hakuweka bayana ni majengo yapi aliyoyaelezea kwamba
yanavuja.Tunapenda kuuhakikishia umma wa watanzania kuwa sio kweli kwamba
majengo ya UDOM yanavuja.Mwandishi alichokiita kuvuja kwa majengo ni
mtiririko wa maji yaliyopo kwenye matenki juu yanapojaa.****
3.Jambo lililozungumziwa na mwandishi kwamba Makamu Mkuu wa Chuo aliwaeleza
viongozi wa serikali waliokitembelea Chuo tarehe 16 Aprili 2011 kuwa Uongozi
unatumia muda ambao wanafunzi wanakuwa likizo kufanya ukarabati mdogo mdogo
ni jambo la kawaida kwa majengo mapya kwani majengo mengi bado yapo kwenye
“defect liability period” hivyo basi kufanyiwa ukarabati mdogo mdogo mara
tu yanapoonekana kuwa na tatizo. Naomba kuweka bayana zaidi hili kwamba ni
ukarabati mdogo mdogo ambao uko ndani ya “defect liability period”.****
4.Makala pia ilielezea kwamba Mifuko ya hifadhi ya jamii iliyojenga Chuo
haina mkataba maalum waliyowekeana na Chuo na akatupa lawama kwa uongozi
wa Chuo kwa kutofanya hivyo.Ukweli ni kwamba Serikali kupitia wizara ya
fedha ndio wenye mamlaka ya kuingia mikataba na Mifuko husika .****
5.Kuhusu kudhulumiwa kwa fedha za wafanyakazi kama ilivyoeleza makala ni
kwamba kama mwandishi alikuwa anafuatilia vizuri suala hilo, serikali
kupitia mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali alifanya ukaguzi wa hesabu za
Chuo na hakukuwa na taarifa za mfanyakazi yoyote aliyedhulumiwa fedha yake
na uongozi wa Chuo.****
** **
6.Mwanchishi pia alihitimisha makala yake kwa kueleza kuwa Chuo kimekuwa
uwanja wa mazoezi kwa polisi.Ukweli ni kwamba Uongozi wa Chuo hauwezi kukaa
kimya wanapoona hali ya amani na usalama wa mali za umma unatetereka.Hali
hii inapotokea kunakuwa na ulazima wa kuwasiliana na vyombo husika ili
kurudisha amani.****
Tafadhali naomba kupitia gazet lako uweke sawa taarifa hii kwa ajili ya
maslahi ya jamii ****
Nakala kwa:*Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi*
* Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo*
* *
*IMETOLEWA NA BEATRICE BALTAZARY*
* AFISA MAHUSIANO *
* CHUO KIKUU CHA DODOMA *
* ** 14 AGOSTI, 2011*
* *Simu ya mezani: *26 2310171
* Simu ya mkononi:*0767 694999*
** **
*
*