“Tanzania ni yetu wote haijalishi upo katika nafasi gani ikiwaka moto itawaka…”

Bernard Baha Kususu Mjadala wa Bajeti ya Ardhi: Nimefuatilia kwa karibu
mjadala wa Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi na hasa kilio cha
wabunge walio wengi kuhusiana na mashamba yaliyotelekezwa na ama ambayo
wawekezaji au wanaoitwa wawekezaji badala ya kuyaendeleza sasa wanayakodisha
kwa wananchi jirani na mashamba haya ambao bila shaka wangekabidhiwa
wangeyaendesha pasi na shaka.

Nimefuatilia pia suala la uwekezaji katika ardhi na nimemsikiliza Mh Waziri
Mkuu akijitahidi kulifafanua hili hapa na pale kwa kazi kubwa kwelikweli.
Kwanza nimpongeze Waziri wa Ardhi kwa kukiri juu ya udhaifu katika sheria ya
marekebisho ya sheria za ardhi ya 2004 kimsingi ubidhaafishaji wa ardhi
ulianza na marekebisho haya sasa kama kuna nia ya dhati ya kutafuta ufumbuzi
wa matatizo hapo ndio haswa pa kuanzia.

Nadhani ufike wakati sasa suala la uwekezaji liwekwe wazi na kuwe na mjadala
wa kitaifa haitoshi tu kuchukua takwimu na kuzieleza kama alivyojitahidi
kufanya huyu kiongozi wa shughuli za serikali bungeni,suala la kujiuliza
kama kweli pana kiasi chote hicho cha mamilioni ya hekta za ardhi
zisizoendelezwa iweje leo kuwe na migongano kati ya wawekezaji na
wanakijiji?

iweje leo tuendelee kuwa na migogoro baina ya makundi ya wafugaji na
wakulima? iweje leo serikali ilazimike kulipa fidia kwa wananchi ili wapishe
wawekezaji?kwanini wawekezaji hawa wasipelekwe kwenye hizo hekta tupu!
ukweli ni kwamba katika kujenga hoja yake hii kajipinga mwenyewe…hivyo
ndio kusema uhalisia wa mambo hakuna ardhi isiyokuwa na mwenyewe na kama
lengo ni kubadilisha kilimo chetu kiwe na tija na hivyo wabakie asilimia 10
hadi 15 ya wakulima na sehemu kubwa iingie katika sekta nyinginezo sidhani
kama hii ni suala la kuamka asubuhi na kukuta muujiza na haitoshi kuamini
kuwa kwa ujio wa wawekezaji itakuwa an overnight process…..

Tuendelee kulitafakari hili,nchi hii ni yetu wote haijalishi upo katika
nafasi gani ikiwaka moto itawaka na wewe ikineemeka itaneemeka na wewe, nini
kifanyike ili kuwe na uwiano kati ya tukipatacho kutokana na michakato hii
ba tunachokitoa.

Jioni njema.

__._,_.___