Temeke kumenoga:  Akili ya Pesa Challenge

Na Maida Waziri, Temeke, Dar es Salaam 12  July, 2022

Ndugu zangu,

Tunapoleta  shindano la Akili ya Pesa Challenge katika wilaya yetu ya Temeke  tumelenga kuhakikisha kwamba vijana wanatumia  msuli  wa wilaya yetu kuvuna hela kiuendelevu.

Hii maana yake  tunategengeneza  uelewa kuhusu fursa zilizopo katika wilaya hii ambazo ni za aina ya pekee.

Ndio! huo ndio ukweli wa Temeke!

Kwani  nani asiyejua kwamba Temeke ni kitovu cha upatikanaji wa uhuru wa Tanzania bara.

Na kwamba Temeke pia ni kitovu cha kwa ukuaji wa michezo, utamaduni na maendeleo ya kilimo, wizara ya kilimo kwa miaka mingi na maabara zake a uchunguzi zipo katika wilaya ya Temeke.

Kwa kuleta shindano  Akili ya Pesa Challenge, Temeke tuna -wachallenge, vijana wa Temeke wanaotaka kupigania uhuru wa kiuchumi .  

Kwa hakika Manispaa ya Temeke ni moja ya Halmashauri chache kongwe yenye utajiri na historia ambayo imechangia kuleta mabadiliko kisiasa, kiuchumi na kijamii nchini.

Tuseme ukweli,Dar-es-Salaam ni Temeke kwa kuwa mambo makubwa yaayochangia kipato cha taifa na burudani yapo.

Ndugu zangu,!

Bandari ipo Temeke, viwanja vyote vya mipira kitaifa – Uwanja wa Taifa na Uwanja wa Uhuru, Azam Complex  na pia  jirani na Uwanja wa ndege wa kimataifa, ni mwanzo wa Reli ya Tazara, ina Uwanja wa kimataifa wa maonyesho – sabasaba, ina daraja la Nyerere ambalo ni la kimataifa.

Katika yote hayo kinacho stahili ni vijana kuunganisha raslimali zilizopo na changamoto ya kujibadili kiuchumi.

Fikiria,samaki hupatikana kwa wingi Temeke, na wilaya hii hii  ina fukwe nzuri za kuvutia zenye mchanga mweupe, minada mikubwa ya Mbande, Vituka na pia masoko maarufu ya matunda na mchele.

Yaaanii hii ndiyoTemeke tunayoisema leo.

Na hakika ukiangalia yote haya unaona kwamba Temeke kumenoga kwa vijana, huku  Mkuu wake wa wilaya ambaye pia ni kijana, Jokate Mwegelo akiwa beeti kuhakikisha kwamba anaibua vipaji anavilea na kuvipeleka mbali zaidi.

Wakati umefika kwa vijana kutambua nafasi yao katika maendeleo ya uchumi wa viwanda na hivyo wafahamu ni kwa namna gani ushiriki wao kikamilifu katika shughuli mbalimbali za uchumi wa viwanda utawasaidia kutoboa.

Ndugu,

Faida ya Ushiriki wa Akili ya Pesa Challenge sio tu kujipatia fedha bali kujipambanua katika kubainisha changamoto mbalimbali zilizopo katika kushiriki kikamilifu kwenye uchumi wa viwanda  ambao serikali ya awamu ya Sita ya Mama Samia Suluhu Hassan anaipigania.

Na hii ndio Akili ya Pesa Challenge

Tunapotafakari tunatambua kwamba  kwa kuzingatia Akili ya Pesa Challenge vijana wanabaki kuwa kitovu cha ubunifu na tija, katika ujasiriamali kwa kukuza mwamko wake.