TANZANIA: Viongozi achene tabia ya kulalamikabalitafutenimajawabu ya kero za wakulima na wafugaji

“SITAKI VYAMA VYA USHIRIKA LIA LIA RUKWA” – RC MKIRIKITI

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Mhe. Joseph JosephMkirikiti amewatakaviongoziwavyama vya ushirikawawilaya za Sumbawanga, Nkasi na Kalambo kuachatabia ya kulalamikabadalayakewahamasisheushirikaunaolengakuchangia kwenye ukuaji wauchumi wa wananchi.

Mkirikiti ametoaagizo hilo leo (03.09.2021) mjini Sumbawanga alipokutana na viongozi wa Chama Kikuu cha UshirikaUfipa cha Rukwa (UCU) pamoja na wanachamawake 60 kujadili changamoto za madeni na ushirikakutokidhimalengo ya wanachama.

“Ushirika li alia haunanafasi kwenye mkoa wa Rukwa kwani Serikali ya Awamu ya Sita inataka kuona wanaushirikawakinufaika na vyamavyao , hivyo Viongozi achene tabia ya kulalamikabalitafutenimajawabu ya kero za wakulima na wafugaji” alisema Mkirikiti.

Mkuu huyo wa Mkoa alibainisha kuwa Ushirikaunahistoriailiyotukuka kwani kupitia ushirikawatoto wa masikiniwalipata elimu na kuchangia maendeleo ya taifa na familiazao dhidi ya umasikini hivyo uwepo wa chamakikuu cha uShirikaUfipauwe ni suluhisho la kuleta maendeleo kwa wana Rukwa siyo migogoro na madeni.

“Wakati mkulima wa Rukwa analalamikakupanda kwa gharama za pembejeo na kukosamasoko ya mazao hapo ndipo Viongozi wa vyama vya ushirikawanapotakiwakubunisuluhisho na kuwasaidiawananchamawao“ alisisitiza Mkirikiti.

Katika hatua nyingine Mkirikiti amesema uwepo wa Chama kikuu cha UshirikaUfipa (UCU) usaidiewakulima ,wavuvi na wafugaji kupata pembejeo ,masoko pia mitaji ili wanachamawapatefaida na kukuzauchumiwao.

Kuhusu tatizo ukosefuwasoko la mahindi na mazao mengine Mkirikiti amesemaviongozi wa ushirikawanalojukumu la kutafuta taarifa za masokokilasiku na kuwafikishiawanachamawao.

Akijibu ombi la Chama kikuu cha ushirika kuhusu Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula kuongeza kiwango cha tani zaununuzimahindi ,Mkirikiti alisema haitowezakununuamahindiyote kutokana na kusudi la serikali.

“NFRA ni taasisi ya kimkakati ya kuhakikishataifalinakuwa na usalama wa chakula ,hivyohaiwezikununuamahindiyote ya wakulima” alisema Mkirikiti.

Akizungumza kuhusu utendajikazi wa Chama Kikuu cha UshirikaUfipa Rukwa ( UCU) Mwenyekiti wake AdabethMbuyani alisema changamoto kubwainayokabiliushirika ni ukosefu wa masoko na gharamakubwa za pembejeo .

Akizungumza kwa niaba ya Tume ya Maendeleo ya Ushirikatoka Makao Makuu ,MrajisMsaidizi Robert George alisema wamefika Rukwa ili kushiriki kikao hicho na kutambua changamoto za wananushirikikufuatia uwepo wa malalamikomengi.

Robert aliongeza kusema uhaiwachama cha ushirikaunatokana na uwepo wa mitaji hatua itakayosaidiachama kuwa na uwezo wa kutoa huduma ikiwemopembejeo na masoko ya mazao.

“Nguvu ya ushirikainatokana na wanachama wenye hisa za kutoshandio maana tunahamasishavyama kuwa na mitaji hatua itakayosaidia kuwa na nguvu za kiuchumikuweza kutoa huduma kwa wadau wake “ alihitimishaMrajisMsaidizi huyo kutoka Dodoma.

Kikao hichoni cha kwanza cha Mkuu wa Mkoa huyo chenye lengo la kufufuauhai wa vyama vya ushirika ambapo kimehudhuriwa na taasisi za fedha za NMB,CRDB,TADB, Eliagro, HELVETAS pamoja na Maafisaushirika wa wilaya za Sumbawanga, Nkasi na Kalambo.