Tanzania inakusudia kuwatumia wataalamu wa Kitanzania walioko Diaspora

KUWATUMIA WATAALAMU WA KITANZANIA WALIOKO UGHAIBUNI (DIASPORA)
NA NDANI YA NCHI KUJENGA UWEZO NA UFANISI WA UTEKELEZAJI WA SHUGHULI
MUHIMU ZA SERIKALI
______________________________

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inakusudia kuwatumia
wataalamu wa Kitanzania walioko ndani ya nchi na wale walioko
ughaibuni (Diaspora) katika kutekeleza mipango yake kadhaa yenye
umuhimu kwa Taifa.

Hapo awali, Serikali iliwatumia zaidi wataalamu kutoka nchi nyingine,
ambapo kwa sasa lengo ni kuona kwamba wataalamu wa nchi nyingine
wanatumika pale tu ambapo wataalamu wa Kitanzania walio ndani na nje
ya nchi hawajapatikana kufanya kazi husika.

Katika kutekeleza azma hiyo, Serikali itapenda kupata wataalamu wa
Kitanzania kwenye maeneo yafuatayo:-

(i) Mfumo mzima wa utafutaji, uchimbaji, uongezaji thamani na
usambazaji wa gesi asilia na mafuta.

(ii) Kuimarisha matumizi salama ya Teknolojia ya Habari na
Mawasiliano (TEHAMA) katika kuboresha utendaji wa Serikali na utoaji
wa huduma kwa wananchi.

(iii) Kuboresha utekelezaji wa malengo ya Serikali na kupima matokeo
kupitia mfumo unaokusudiwa kuhakikisha tunapata matokeo makubwa na ya
haraka katika maeneo ya kipaumbele na kimkakati katika maendeleo ya
Taifa.

Wataalamu watakaojitokeza na kukubaliwa kufanya kazi Serikalini katika
maeneo haya, watafanya kazi kwa mikataba ya muda mfupi, lakini
inayoweza kuongezwa iwapo utendaji utaridhisha.

Mwito unatolewa kwa Wataalamu wa Kitanzania popote walipo, ughaibuni
au ndani ya nchi, kujitokeza na kuleta wasifu wao (CV’s) pamoja na
maelezo ya kwa nini wanafikiri wao ni aina ya watu tunaowatafuta.
Tumia anuani ifuatayo:-

Katibu Mkuu Kiongozi
Ofisi ya Rais, Ikulu
S.L.P. 9120
DAR ES SALAAM.

E.mail:chief@ikulu.go.tz
__._,_.___
Reply via web
post
Reply
to sender

Reply
to group

Start
a New Topic
Messages
in this topic(1)
Recent Activity:

Visit Your Group
[image: Yahoo!
Groups]
Switch to: Text-Only,
Daily Digest
Unsubscribe • Terms
of Use • Send us Feedback

.

__,_._,___