Tanzania imepokea msaada bilioni 133 kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika-ADB

SERIKALI YAPATA MSAADA WA FEDHA KUTOKA BENKI YA MAEDNELEO YA AFRIKA
(Na Esther Muze na Bebi Kapenya – MAELEZO)
12.9.2011
Serikali ya Tanzania imepokea msaada wa shilingi bilioni 133 kutoka
Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) kwa ajili ya kusaidia miradi
kuendeleza sekta ya kilimo na elimu nchini.

Msaada huo ulisainiwa jana jijini Dar es Salaam na Waziri wa fedha
Mustafa Mkulo kwa niaba ya Tanzania na Mwakilishi wa Benki ya
Maendeleo ya Afrika Tonia Kandiero.

Akiongea mara baada ya kupokea msaada huo, Waziri wa Fedha alisema
kuwa, fedha hizo zitasidia katika kuboresha sekta ya kilimo ikiwemo
miundombinu ya masoko .

Aliongeza kuwa, sehemu nyingine ya fedha hizo itasaidia kutoa mafunzo
kwa vijana wenye mahitaji maalum ambao walioacha masomo kabla ya
kumaliza elimu yao kwa sababu mbalimbali.

Mkulo aliahidi kuwa Serikali ya Tanzania itahakisha kuwa msaada huo
unatumika katika maeneo waliyokubaliana ili kuleta maendeleo kwa kwa
wananchi na kupunguzia umaskini.

Naye Mwakilishi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB), Tonia alisema
kuwa, msaada uliotolewa na Benki hiyo utasaidia Tanzania kiuchumi
katika harakatio zake za kukuza uchumi na kupunguza umaskini.

Aliongeza kuwa msaada huo utawasaidia vijana kupata ujuzi katika
visiwa vya Zanzibar ambao watasaidia kuongeza nguvukazi katika soko la
ajira kwa ajili ya kuleta maendeleo yao na nchi kwa ujumla.

Aidha alisema kuwa Benki hiyo itaendelea kuisaidia Tanzania ili kukuza
maendeleo yake ya kiuchumi na kijamii.

Benki ya Maendeleo ya Afrika kwa miaka mitatu iliyopita imekuwa ikitoa
misaada ya kifedha kwa lengo la  kuisaidia Tanzania  kiuchumi.

MWISHO


Sent from my mobile device