SUPER D AACHIA DVD TATU ZA KIMATAIFA KUFUNZIA NGUMI

Dar es Salaam:

Kocha maarufu wa mchezo wa ngumi nchini, Rajabu Mhamila ‘SUPER D’ aliyeamua
kutumia njia ya DVD kuwafundisha watu mbalimbali kujua na kutambua sheria za
mchezo huo ameachia kazi nyingine tatu mpya.

Kazi hizo tatu zinausisha mapambano kadhjaaa ya nyota na mabingwa wa ngumi
za kulipwa Duniani, ziliachiwa sokoni zaidi ya wiki moja sasa.

Akizungumza na waandishi wa habari Super D, alisema tofauti na kanda yake ya
awali iliyokwenda kwa SUPER D BOXING COACH, DVD za sasa zimeandaliwa kisasa
na zikiwa na mchanganyiko wa ‘clips’ za michezo ya nyota wa Dunia katika
kuwafunza watu namna ya kupigana ngumi.

Super D, alisema mbali na michezo ya nyota hao wa Dunia akiwemo Manny
Pacquio, Floyd Maywether, Roy Jones na wakali wengine DVD hizo zina michezo
ya tamasha lao la ngumi wanaloendesha kwa kushirikiana na kocha mkongwe
Habibi Kinyogoli.

”katika muendelezo wa kuwafunza watu ngumi kwa njia rahisi, nimetoa dvd
pamoja na CD nyingine tatu tofauti zilizokusanya michezo ya mabingwa wa
dunia na mafunzo ya ngumi tunayoendesha kupitia tamasha letu na Kinyogoli
Foundition ” alisema. Super D ambae ni kocha wa timu ya ngumi ya Ashanti
pamoja na timu ya mkoa wa Ilala kimichezo alisema anamini kupitia njia watu
wengi wenye kupenda kujifunza mchezo wa ngumi kwa kuangalia mbinu na ufundi
katika mchezo huo kupitia michezo ya mabondia waliopo kwenye dvd hizo.

Aliongeza kuwa, mbali na dvd hizo bado wanaitajika vijana wenye vipaji
kujitokeza kuja kushiriki katika mazoezi ya ngumi ili wajiunge na wenzao wa
timu ya Ashanti na Amana kujifunza ‘live’ chini ya makocha Habibu Kinyogoli,
Kondo Nassoro, na yeye mwenyewe Super D na wengine wanaowanoa vijana
mbalimbali