NGUMI KULINDIMA ILALA Oktoba16

ZAIDI ya mabondia 42 wanatarajia kushiriki katika mashindano ya mchezo
wa ngumi yanayotarajiwa kufanyika Oktoba16 mwaka huu Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kocha wa Klabu ya Ashanti ya
Ilala, Rajabu Mhamila, ‘Super D’ alisema kuwa mashindano hayo
yanatarajiwa kushirikisha Klabu 12 kutoka katika maeneo mbalimbali.

Alisema kuwa mashindano hayo yanatarajia kufanyika katika ukumbi wa
Panandi Panandi Ilala.

Super D alisema kuwa mashindano hayo yana lengo la kuhendeleza
kuhamasisha mchezo wa ngumi nchini ikiwa ni pamoja na muendelezo wa
mchezo huo unanaofanywa na Kinyogoli Foundation.

“Tumeandaa mashindano ya ngumi ambayo yatashirikisha vijana mbalimbali
na lengo letu ni kuhamasisha mchezo huo ikiwa ni pamoja na kuuendeleza
ili uweze kutuletea faida hapo baaye” alisema.

Kocha huyo alisema kuwa vijana watakaoshiriki watakuwa katika uzito
mbalimbali kuanzia Unyoya mpaka uzito wa juu.

Alisema kuwa pia wanatarajia kushirikisha mabondia wa kike kutoka
katika klabu hizo hizo

Aliongeza kwa kusema kuwa wanaitaji wadau mbalimbali wajitokeze
kuwasaidia mahitaji mbalimbali ya vijana ikiwemo maji kwa ajili ya
mchezo huo kwa siku hiyo wenye nia ya kutaka kusaidia au kushiliki kwa
kuchangia chochote wanaweza kuja katika ukumbi wa mazoezi uliopo Amana
Ilala au kufika Ashanti Boxingi clabu kwa mawasiliano zai unaweza kuwa
siliana na Kocha Mkongwe, Habibu Kinyogoli kwa simu 0655928298 au
unaweza kuwasiliana na Super D Boxing Coach O713,0787-406938
Email.superdboxingcoach@gmail.com wadau mbalimbali mnakalibishwa