Mhe. Maige ATEUA BODI YA WAKURUGENZI YA BODI YA UTALII

Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Ezekiel M. Maige (MB) kwa Mamlaka
aliyonayo amewateua wajumbe watano kuunda Bodi ya Wakurugenzi ya Bodi
ya Utalii (TTB) kuanzia tarehe 23 Machi, 2012.

Uteuzi huo unafuatia Mhe. Rais Jakaya M. Kikwete kumteua Balozi
Charles A. Sanga kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya TTB mapema wiki hii.
Walioteuliwa kuwa Wakurugenzi wa Bodi hiyo itakayodumu kwa miaka
mitatu ni pamoja na:-

1. Prof. Isaya Jairo PhD, Mhadhiri wa Biashara na Uchumi, Chuo cha
Usimamizi wa Fedha, IFM;

2. Ndugu Teddy Mapunda, Mtaalamu wa Masoko (Marketing) na Afisa
Uhusiano Serengeti Breweries Limited;

3. Ndugu Samwel D.I. Diah, Mtaalamu na Mdau wa Biashara na Utalii na
Mkurugenzi Mwendeshaji wa Kampuni ya Tanzania Travel Co. Limited;

4. Mhe. Kaika S. Telele (Mb), Mbunge wa Ngorongoro na Mdau wa Utalii na;

5. Mhe. Abdulkarim Shah (Mb), Mbunge wa Mafia na Mdau wa Utalii.