Mawaziri: Rais hajapata taarifa yeyote rasmi kutoka kwa Waziri Mkuu

Ikulu inapenda kukanusha taarifa zilizonukuliwa na baadhi ya vyombo
vya habari kudai kuwa Rais ametofautiana na Waziri Mkuu kuhusu aina ya
hatua za kuwachukulia Mawaziri wanaotuhumiwa na ubadhirifu katika
Wizara zao.

Napenda kueleza Umma kuwa taarifa hizo si za kweli.
Pia  nitumie nafasi  hii kuwatahadharisha waandishi wa habari  kuwa
makini, waangalifu na wachambuzi wakati wa kupokea, kusikiliza na
kuandika au kutangaza taarifa wanazopata.

Rais kikwete aliwasili kutoka Brazil alipokuwa amekwenda Kwa Ziara ya
kikazi ya siku tano tarehe 21 April, 2012.

Kwa hivyo basi Rais hajapata taarifa yeyote rasmi kutoka kwa Waziri
Mkuu, na bado anasubiri kupewa taarifa hyo rasmi Kwa vile suala la
tuhuma hizo limetokea Bungeni.

Na kama kuna Waziri ambaye ameandika barua ya kujiuzulu, basi atakua
amemuandikia Rais na kama zipo Rais ndiye atakaye zipokea na kuamua
hatua inayofuatia.

Kwa hivyo sio busara hata kidogo kwa vyombo vya habari kueneza uongo
na fitna zenye lengo la kuchonganisha si viongozi tu , bali  hata
viongozi na wananchi kwa ujumla.

Rais Kikwete anatarajia kurejea nchini kesho  tarehe 23 April mara
baada ya maziko.
………………………..

Mwisho ………………

Imetolewa na Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais, Msaidizi
Blantyre -Malawi.
22 April, 2012


Sent from my mobile device