Deogratias Sarufu:
Chanzo cha mufumuko wa bei
hapa nchini ni chakula. Wataalamu
wa
uchumi wa Benki kuu ya Tanzania wanasema iwapo bei ya
chakula
itapungua, mfumuko wa bei nao hupungua. Ukweli huu
unaambatana na
ukweli mwingine kwamba taifa hili asilimia 80 ya watu wake
ni wakulima
wadogo wanaokabiliwa na changamoto nyingi zinazosababisha
kuzalisha
nafaka kidogo na hivyo kuleta uhaba wa chakula
nchini.Deogratias
Sarufu akiandika kwa niaba ya Panos East Africa anazungumzia
changamoto za mkulima wa Tanzania kwa kuangalia moja ya
mikoa
inayolisha Tanzania, Morogoro.
Kwa nchi ambayo kukua
kwa uchumi wake kunategemea zaidi uwapo wa
chakula kwa kubadili kilimo ili kifikie angalau mchango wa
asilimia 20
wa pato la taifa matumizi ya pembejeo katika kuinua ni lazima.
Mkoa wa Morogoro ni mojawapo ya mikoa ambayo inalisha
Tanzania na
umetamkwa wazi na rais Jakaya Kikwete kuwa ghala la
kuhifadhia chakula
la taifa. Mikoa mkingine ambayo inategemewa kwa nafaska ya
chakula ni
Ruvuma,Mbeya, Iringa na Rukwa.
Kutokana na umuhimu wake kwa taifa mkoa huu umeingizwa pia
katika
mpango wa kupewa vocha za pembejeo za ruzuku yaani mbolea ya
kupanda
na kukuzia na mbegu bora .
Mkoa wa morogoro ambao umebarikiwa kuwa na mabonde ya kilimo
na
umwagiliaji ,kilimo chake kwa miaka mingi kimeachwa kujiendesha
chenyewe
japo ndicho kinachotegemewa na asilimia 80 ya wananchi. Kwa
kilimo
mkoa huu bado unategemea mkulima mdogo, anayetegemea jembe
la mkono
akiwa na maarifa
kidogo au yasiyotosha kuhusu
kilimo
chenyewe.Kimsingi kilimo cha Tanzania kwa miaka mingi
kimekuwa
kikikosa teknolojia na sayansi ya kilimo yaani matumizi ya
mbolea na
viuatilifu na pia utashi kutoka kwa viongozi ulikuwa wa
kutia shaka.
Ili kukibadili kilimo cha Tanzania kama ilivyokusudiwa ipo
haja ya
kuwabadili wakulima kama alivyosema mshauri kilimo wa mkoa wa
Morogoro Bi.Aulalia Minja .
Mshauri huyo alisem a kwamba wakulima wa mkoa wake
wanakabiliwa na
changamoto kubwa ya kutekeleza agizo la Rais Kikwete kuwa
ghala la
chakula kwa kuzingatia gharama kubwa za kilimo na kipato
kidogo
kinachoambatana nacho.
Pamoja na gharama hizo kwenye pembejeo licha ya serikali
kutoa ruzuku
kw abaadhi ya wakulima, matumizi ya mbegu bora bado ni
tatizo.
“Hapa nchini matumizi ya mbegu bora ni chini ya asilimia 10 ,kiwango
ambacho ni kidogo sana ukilinganisha na nchi zingine za
Afrika.Tatizo
hilo lipo na hapa
mkoani mwangu” alisema Bi Minja.
Mkulima wa Morogoro na changamoto zake hajatofautiana na
wakulima wa
wengine wa Tanzania ambao ama hakika wanakabiliwa na
changamoto
lukuki,kama upatikanaji
wa mbegu bora .
Morogoro ambayo ni sampuli nasibu kuzungumzia wakulima wa
Tanzania
yenye zaidi ya kilomita za mraba 900,000 ni mkoa wenye kilomita za
mraba zipatazo 73,039 ambazo ni sawa na asilimia 8 ya eneo lote la
Tanzania.Kilomita hizi za mraba zinaupa sifa ya kuwa mkoa wa
pili kwa
ukubwa nchini Tanzania ukitanguliwa na Mkoa wa Tabora.
Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na ofisi ya mkoa wa
morogoro, mkoa
una eneo la hekta zipatazo 123,507 zinazofaa kwa kilimo.Hata
hivyo kwa
mujibu wa taarifa zilizopo mpaka sasa ni hekta 8,804 pekee ndizo
zinazotumika kwa kilimo.
Kama ilivyo kwa mikoa mingi nchini Tanzania,zaidi ya
asilimia 80 ya
wakazi wapatao 1,759,809 Mkoani humo ni wakulima.
Nikiwa Ofisi ya mshauri wa masuala ya kilimo mkoani humo,Bi
Aulalia
Minja alisema kwamba pamoja na ufinyu wa eneo linalotumika
kwa kilimo
bado kilimo hakijaleta tija inayotakiwa ambayo ingelimuondoa
mkulima
wa morogoro kutoka katika lindi la umaskini kutokana na
udhaifu katika
kilimo chenyewe kutokana na kukosekana kwa matumizi ya
kutosha ya
pembejeo na pia kuacha kutegemea mvua kwa ajili ya kilimo.
Kwa mujibu wa mshauri wa kilimo mkoa wa Morogoro Bi.Aulalia
Minja
katika msimu wa kilimo wa mwaka 2010/2011 mkoa huo ulihitaji
tani
14,198.4 za mbegu bora ikiwa ni moja ya jitihada za
kuhakikisha kuwa
mkoa unakuwa na chakula cha kutosha,lakini pia unaongeza
pato la
mkulima ili kupunguza kama sio kuondoa kabisa umasikini.
Mahitaji hayo ya mbegu bora ni kwa mazao ya
mahindi,mpunga,mtama,maharage,kunde,mbaazi, ,alizeti na
ufuta.
Hata hivyo tofauti na ilivyotarajiwa,lengo la mahitaji hayo
ya mbegu
bora halikufikiwa mkoani humo kutokana na kupatikana kiasi
kidogo cha
mbegu,ambapo kati ya tani14,198.4 za mbegu bora zilizokuwa
zikihitajika 2010/2011 ,ni tani 1,457.06 pekee za mbegu
ndizo
zilipatikana ikiwa ni takribani asilimia 1 ya mahitaji stahiki.
Afisa huyo alifafanua kuwa kiasi hicho cha mbegu bora
kilikuwa ni cha
ruzuku kwa mazao ya
mpunga na mahindi,ambapo kwa upande wa mahindi
mbegu zilizopatikana ilikuwa ni tani 1,307.06 na mpunga
ilikuwa ni
tani 150 pekee,ikiwa ni sawa na kila wilaya kupata wastani
wa tani 242
za mbegu bora.
Watu maarufu wa
uzalishaji wa mbegu za mahindi Tanseed International
Ltd,moja ya makampuni yanaozalisha mbegu bora za mahindi
aina ya Tan
250,Tan 254,Tan H611,Tan 600 na Tan222 wanasema kwamba
mahitaji kwa
sasa yanazidiwa na uzalishaji unaofanyika katika mashamba ya
mbegu!
Kwa mujibu wa maelezo ya Meneja wa Tanseed International
Ltd,Bw Isaka
Mashauri,pamoja na kutotaka kutaja kiasi cha tani
kinachozalishwa na
kampuni yake alisema pia kuwa uhaba wa mbegu unachangiwa na
gharama za
uzalishaji kuwa juu,hivyo kutoa wito kwa serikali
kuwapunguzia kodi
makampuni binafsi yanayozalisha mbegu bora ili waweze
kuzalisha mbegu
hizo kwa wingi na kukidhi mahitaji ya wakulima.
Maelezo hayo yalitoa mwanga kwamba kuna uzalishaji mdogo wa
mbegu bora
kwa kila mkulima na kufanya moja ya changamoto kubwa ya
mkulima wa
Tanzania kuwa upatikanaji wa mbegu bora.
Kwa upande wa wakulima tatizo kwao si kupatikana kwa mbegu
bali bei
kubwa ya mbegu hizo: kutokana na kuwapo kwa utata juu ya
changamoto
hasa ya wakulima kwenye mbegu bado ukweli unabaki kwamba
mkulima mdogo
hatumii mbegu bora kwa sababu tofauti japo uhaba unachangia.
Sehemu kubwa ya tatizo lake ni ughali wa mbegu na uwezo duni
wa
kununua mbegu hizo.
Wakulima wa Mikese na
Ngerengere walipozungumza na mwandishi wa
habari hizi walisema wazi kwamba changamoto inayowakabili
wao katika
suala la upatikanaji wa mbegu bora ni bei kubwa.kwa mujibu
wa wakulima
hao hata kiasi kidogo cha mbegu bora kinachopatikana
sasa,wao bado
hawezi kukipata kutokana na kuuzwa kwa bei wasiyoweza kuimudu.
Walisema kwa sasa mfuko wa mbegu bora za mahindi wenye ujazo
wa kilo 2
unauzwa kwa gharama ya shilingi za Kitanzania 4,000;ambapo
ili kuweza
kupata mbegu ya kutosha ekari moja zinahitajika kilo 6
ambazo ni sawa
na shilingi 24,000.
“Ndugu mwandishi mfuko mmoja wa mbegu bora wenye ujazo wa
kilo2
unauzwa 4,000/=na ili niweze kupanda ekari moja nahitaji
kilo 6 ambazo
ni sh 24,000 Siwezi kumudu gharama hizo,ni bora nikanunue
mbegu za
asili ambazo kwa kilo 18-20 nauziwa kwa gharama ya
6,000/=ambapo
naweza kutumia mbegu hizo kwa ekari moja” alisema mmoja wa
wakulima
Bw..Said Mchaga
Changamoto nyingine inayotajwa na wakulima hao ni baadhi ya
mbegu bora
kukosa ladha waliyoizoea,walisema kuwa baadhi ya mbegu bora
hazina
ladha nzuri ya asili waliyoizoea hasa wanapokula mahindi ya
kuchoma au
kuchemsha.
“Kusema ukweli mahindi haya ya mbegu za kisasa hayana ladha
nzuri
kabisa unapoyala yakiwa yamechomwa au kuchemsha
ukilinganisha na yale
yaliyopandwa kwa mbegu za asili.Labda kwa ugali,labda!”
alisema Bw.
Abdala Siali wa kijiji,cha Ngerengere.
Wakati mwingine unashangaa falsafa ya mkulima kuhusiana na
suala hilo
la ladha ambalo wakati mwingine linamfanya asifanye juhudi
za kutafuta
mbegu hizo bora kwa kuwa hazina ladha.
Hata hivyo wakulima
wameelezea changamoto nyine ambapo inaonekana
baadhi ya mbegu hukosa ubora wa matumizi ya kilimo.Kwa
mujibu wa afisa
ugani wa Kijiji cha Mikese,Bibi Kilonzo Mbwambo wakulima
wamekuwa
wakimwendea mara nyingi kulalamika juu ya kushindwa kuota
kwa mbegu
zilizoaminika kuwa ni bora mara baada ya kupandwa ardhini na
muda wake
wa kuota kuwadia.
Alisema kuna
uwezekano wa kuwepo kwa baadhi wafanyabiashara wasio
waaminifu wa maduka ya pembejeo za kilimo ambao huwauzia
wakulima
mbegu zilizokwisha muda wake wa matumizi ya kilimo kwa lengo
la kupata
faida kinyume na utaratibu.
“ipo sheri aya kushtaki watu hawa dawa ni kw awakulima kunua
mbegu
katika maduka ya pembvejeo wadai risiti ili kunapotoke
amushkeri
tuweze kufuatilia.” Alisema bibi shamba huyo .
Aidha alitaka wakulima kuzingatia majaribio ya uotaji wa
mbegu mpya
ambazo wanazipata kwa kuzifanyia majaribio stahiki.
Hata hivyo afisa ugani huyo alisema kuwa ili kuepukana na
tatizo hilo
huwashauri wakulima kijijini hapo kuwa na tabia ya kununua
mbegu bora
mapema na kisha kuzipanda chache kwa majaribio ili kama
hazitaota
waweze kuchukua tahadhari mapema.
Jinsi changamoto za upatikanaji wa mbegu bora mkoani humo
zilivyobainishwa na wakulima na wadau wengine,nidhahiri
kwamba wadau
wa sekta ya kilimo hususani Wizara ya kilimo,wazalishaji wa
mbegu bora
pamoja na wakulima wanatakiwa kushikamana ili kuhakikisha
kwamba mbegu
bora zinapatikana kwa wingi na kwa gharama nafuu.
Hayo yote yakifanyika jitihada za kuufanya mkoa wa Morogoro
kuwa ghala
la chakula la taifa pamoja na jitihada za kutekeleza sera ya
kilimo
kwanza yenye lengo la kutekeleza mkakati wa kukuza uchumi na
kupunguza
umasikini Tanzania (MKUKUTA) litafikiwa.
Ni wazi kuwa kunahitajika
juhudi za makusudi kwanza kubadili fikira
na kupima kw auzito unakubalika juu ya umuhimu wa mbegu bora yenye
ujazo mkubwa bila kujali ladha hasa kwa ajili ya kuongeza
kipato na
kuanzisha mfumo wa kuweka akiba ili kumudu kununua mbolea na
pembejeo
nyingine kwa ajili ya kufanya mapinduzi ya kilimo.
Katika suala la ruzuku Minja alisema kwmaba serikali
imepeleka kwa
muda unaostahili
vocha hizo japo maeneo mengtine ya mkoa wa Morogoro
walanguzi wametokea na kuvuruga mfumo kwa kuwarubuni wa
kulima.
“Wapo wakulima kama katika eneo la mvomero na pia kilosa
wamekuwa
wakipewa fedha kidogo na kuuza vocha hizo hali ambayo
inaleta shida na
kuchelewesha mabadiliko miongoni mwa wakuloima wetu.”
Alisema Minja.
Morogoro ambayo ni miongoni mwa mikoa kadhaa inayopewa
ruzuku ya
pembejeo imekuw aikikabiliw ana ufiosadi wa ajabu wa
matumizi mabaya
ambapo wakulima wandanganywa kukubali shilingi cache kwa
kutoa hatiz a
ununuzi wa pembejeo kumbe hawakununua na hivyo mashamba
kukosa mblea
inayohitajika na mbegu zinaozstahili.
Kwa hiyo tatizo si mbegu tu na fikira zao bali pia na
Mawakala ambao
kwa kushirikiana na viongozi wengine wasiokuwa waaminifu
wamekuwa
wakijilipa vocha bila kutoa huduma.
Mawakala wamekuwa hodari mno kubuni mbinu ya kulaghaia
wakulima
maskini na kuwafanya wakubaliane nao, wakidhani wanapata
kumbe wamepatikana.
Vocha ya ruzuku katika pembejeo ni mkombozi kwa jamii , angalau kama
sehemu ya kilimo darasa na pia kuwezesha wakulima maskini
lakini kwa
mtindo wa ulaghai unaojitokeza inakuwa taabu kubwa kubadili
maisha ya
wakulima.
“Kuna tatizo la mawakala kuweka bei ya juu sana ya
mbolea na hata
mbegu” alisema mmoja wa wakulima Madenge na kuongeza
kwamba kutokana
na hali hiyo ni vyema
mawakala wakabanwa na kuwa na mtazamo sawa na
serikali wa kusaidia wakulima kuondokana na umaskini.
mwisho