ASKARI WA WANYAMAPORI AMEUWAWA NA MAJANGILI KATIKA PORI LA AKIBA LA MASWA

Dar es Salaam:

Wizara ya
Maliasili na Utalii inasikitika kutoa taarifa kwa umma kuwa tarehe 03/01/2012 mnamo
saa 6.20 usiku, askari wa Wanyamapori aitwaye Dorcas K. Rumbagi alipigwa risasi
na watu wanaosadikiwa kuwa ni majangili katika Pori la Akiba la Maswa. Marehemu
alifariki njiani alipokuwa akipelekwa hospitali.

Mwili wa marehemu ulisafirishwa kwenda Kibara – Bunda mkoani Mara ambako alizikwa
tarehe 6/01/2012.

Taarifa kuhusu kitendo hicho cha mauaji ya askari
wa wanyamapori ilitolewa katika Kituo cha Polisi cha Meatu na hadi sasa
watuhumiwa kumi wameshakamatwa na wanaisaidia polisi.

Wizara inachukua fursa hii kuwaomba wananchi
wanaoishi karibu na Pori la Akiba la Maswa, na sehemu zingine, kutoa
ushirikiano ili waliohusika wote na mauaji hayo waweze kukamatwa.

Wakati huohuo Wizara imeongeza askari katika Pori
la Akiba la Maswa ili kuimarisha ulinzi.

George Matiko

MSEMAJI

WIZARA YA
MALIASILI NA UTALII