Na Anna Ruhasha:
TAKWIMU zinaonesha kwamba kuna tatizo kubwa la kutoa elimu kubadili
wakulima wa mpunga hasa kwenye wilaya ya Kilombero.
Hali hiyo inatokana na ukweli kuwa kati ya asilimia 80 ya wakulima
waliopatiwa elimu ya uzalishaji ni asilimia 30.1 walionekana kuwa na
mwelekeo wakati asilimia 49 hawana elimu ya uzalishaji .
Aidha asilimia 30.1 ya wakulima waliopatiwa elimu ya uzalishaji wa zao la
mpunga ndio wamejiunga kwenye vikundi vilivyopo wilaya ya Kilombero
mkoani morogoro.
Takwimu za kijiji cha Mwaya Kilichopo Kata Mwaya Tarafa ya Mang’ula
Wilayani Kilombero Mkoani Morogoro,zinathibitisha kuwapo kwa tatizo hilo la
elimu.Wataalamu wanasema kwamba kukosekana kwa elimu ya zao hilo kwa
asilimia 70 kuchangia kushuka kwa uzalishaji wa mpunga wilayani humo.
Takwimu zinaonyesha asilimia 70 wakulima wadogo hupata kati ya gunia 3
hadi 6 kwa hekari moja ambapo hutumia kilo 30 hadi 40 za mbegu wakati
wakipanda kienyeji kwa kumwaga mbengu .
Asilimia 10 ya wakulima waliopatiwa elimu ya kilimo cha mpunga kwa kufuata
majira ya mvua ambao hupanda mbegu badala ya kumwaga ,huvuna kati ya gunia
22 hadi 30 kwa hekari.
Na wakulima ambao hupandikiza kwa kufuata elimu hupata kati ya gunia 37
hadi 48 kwa hekari moja,
Kwa matokeo hayo inaonekana dhahiri kwamba endapo serikali ingetoa elimu
ya uzalishaji na kuongeza upatikaji wa teknolojia kwa urahisi, kupata
mbegu bora za mpunga, wakulima wadogo, wangeweza kuleta mabadiliko
chanya katika kuongeza chakula nchini.
Kauli hiyo pia imetolewa na asasi isiyo ya kiserikali ya RUDi yenye
kuunganisha wakulima wa vijijini.
Taarifa imesema kwamba pamoja na gharama zote hizo bado mkulima anauza
gunia la mpunga lenye ujazo wa kilo mia moja shilingi elfu 45000.
Diwani wa kata hiyo anasema endapo wakulima wakipatiwa elimu nzuri
watakayo itumia katika kilimo itawasaidia kuondokana na gharama kubwa
wanazozitumia na kuongeza mnyororo wa thamani
Afisa kilimo wa halmashauri ya wilaya ya kilombero Maria Lesharo alikiri
na kusema mbali na idara yake kukabiliwa na changomoto hiyo alisema kuwa,
uzalishaji wa zao la mpunga mwaka 2013 umeongezeka na kufikia
asilimia 98 kutoka asilimia 85 mwaka 2012 kutona hali ya hewa kuwa nzuri.
Tatizo jingine unaliona katika matumizi ya mashine za kukoboa mpunga.
Katika hali isiyokuwa ya ,imeelezwa kuwa kutokana na biashara za mashine
za
kukoboa mpunga kuwa ngumu, vikundi vya wakulima wa zao hilo wameshindwa
kufanya biashara.
Mashine hizi kutokana na bei ndogo ya mpunga hazifanyi kazi kwani wakulima
wanasubiri bei ipande.
Wakieleza changamoto walizokabiliana nazo katika msimu wa mwaka huu
,wanavikundi hao walisema kuwa biashara za mashine ambazo walipatiwa
kwaajiri ya kufanyabishara na kuongeza thamani ya uzalishaji na kipato kwa
ujumla biashara hiyo imekuwa ngumu.
Suna kulolela Katibu wa vikundi hivyo alisema kuwa wanafanyabishara za
mashine kama vikundi ambapo shughuli hiyo ni baada ya kupewa mikopo na benk
ya CGRT pamoja na mashine za wa fadhili kutoka shirika la USAID lililopo
nchini Marekani chini ya usimamizi wa RUDI asasiisiyokuwa ya kiserikali
inayofanya kazi mjini na vijijini kwa lengo la kutoa Elimu kwa wakulima
,kuwatafutia Masoko, na kuwashauri kuazisha vikoba ili kuongeza thamani
mnyororo wa thamani ya uzalishaji.
Saidi Byabyabya mfanyabiashara wa kijiji cha Mkasu ,anasema ugumu wa
biashara za mashine ni kutokana na wafanyabishara kukata tamaa kununua
mchale mashineni wa kuusafirisha kwenda sokoni kutoka na babadiliko ya bei
ya kila mara .
Kwa upande wake meneja wa shirika la wakulima wa mpunga wilayani
humo(AKILIGO)alisema kuwa pamoja na changamoto wanazokabiliana nazo katika
biashara ya mashine za kukoboa mpunga siyo hizo pekee bali wanakabiliwa na
wanavikundi kutokuwa na elimu ya ujasiliamari hali inayopelekea kushindwa
kushawishi walaji kupata huduma mahali hapo.
Aliongeza kuwa shirika hilo lina jumla ya wanachama12,000 ambapo wanaume ni
98,200na wanawake 57,900 kati yao hao hakuna mwenye elimu ya ujasiliamari
kwani hadi sasa wanatumia uzoefu tu.
Naye afisa masoko katika kikundi cha Mangu’la Kasimu Nandiga alisema kuwa
kupitia vikundi vyao ambavyo walipewa mashine kwa ajili ya kuongeza thamani
ya uzalishaji na kipato kwa ujumla wameshindwa kufanya kazi kutokana na
kushuka kwa bei.
Akitoa ushauri Mtendaji Mkuu Washirikalisilokuwa la kiserikali la
RUDI,lenye makao yake makuu jijijni Dar es-salaam Abely Lyimo wakati wa
ziara yake ya siku moja katika kutembelea vikundi vya ujasiriamali katika
wilaya ya kilombero mkoani humo,alisema wanavikundi wawe wabunifu katika
kufanyabiashara za pamoja.
Hata hivyo uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa habari hizi umebaini kuwa
serikali bado haijazingatia sera ya kilimo kwanza ambayo ni nguzo ya saba
inayosema wakulima waelimishwe kwa kupewa elimu ya kibiashara, pia
changomoto hizo serikali kupitia wizara ya kilimo chakula na ushirika
inaitakiwa kuwajengea uwezo wakulima wadogo kwa kuwapatia elimu ya
ujasiliamali ili waweze kwenda sambamba na mkakati wa kilimo kwanza.
Stakabadhi ghalani
Utafiti kidogo umebainisha kwamba mfumo wa stakabadhi mazaoa ghalani
umekuwa vitega uchumi vya asasi za kifedha kutokana na riba ya mikopo
kupanda kwa asilimia 19 .5 kutoka asilimia 14.0 mwaka 2008 ,na
kusababisha asilimia 45 ya wakulima wa mpunga wilayani kilombero
kutochukua mikopo mwaka 2013.
Wakulima hao wamesema kuwa mbali na kuwepo kwa mfumo huo ambao lengo
kuwasaidia wakulima kupata mikopo kupitia mazao yao, mfumo huo umegeuka
kuwa wakibiashara, baada ya wasimamizi wa maghala na asasi za kifedha
kuendelea kujinufaisha kwa kupitia migongo ya wakulima.
Kwaupande wake Bw.John Ngisa ambaye ni mmoja wa wamiliki wa maghala
amesema kuwa kuyumba kwa bei za mchele kila mwaka kumesababisha
wakulima kukata tamaa katika kuchukua mikopo kwaajiri ya kuhifadhi
mazao,pamoja na mabadiliko ya kilimo cha mpunga ambacho hulimwa mara tatu
kwa mwaka kwa kutegemeana na hali ya hewa .
Naye Bi Zainabu mwenyekiti wa UZINZA SACCOS kata ya mwaya amesema
wakulima hawajaitikia kwa wingi katika kuchukua mikopo kwa mwaka huu
ikilinganishwa na miaka ya nyuma ,kutokana na masharti ya mikopo kuwa
migumu ,ambapo masharti hayo yanamtaka kila mkulima ambaye anachukua mkopo
lazima awe mkulima mdogo napia awe na hisa tano za kumdhamini.
“Hisa tano sawa na gunia tano za mpunga, wanachukua mikopo kama kikundi
kama malipo ya awali wakisubiri bei kupanda ili wauze kwa pamoja na
kurudisha mkopo wenye riba kwahiyo masharti yanawashinda”Alisema Zainabu.
Maiko kahuruda ambaye ni mwenyekiti wa kijiji cha kidatu ,amesema elimu
ya mkopo haijatolewa kikamilifu kwa wakulima wengi,ambapo wanakopa bila
kujua hasara na faida za mikopo
“Mfano utaratibu wa mfumo wa stakabadhi mazao ghalani kila mwanachama
anatakiwa kuwa na hisa tano kwenye ghala ambazo ni gunia tano za mpunga
,hisa hizo hutokana na kukopa kiwango cha fedha au malipo ya awali
ukisubiri bei ya soko ,endapo bei ya soko ikiwa nzuri unapata
faida”.alisema.
Afisa kilimo wa wilaya ya Kilombero Bi Maria lesharo alidai kuwa vikwazo
vyha mikopo vinatokana na ugumu wa masharti ya mfumo wa mazoa
ghalani,malipo ya mikopo isiyo wanufaisha kiuchumi.
Bw.Ibrahimu Mghonu ,mratibu wa asasi isiyokuwa ya kiserikali RUDI
inayofanya shughuli zake mjini na vijijini kwa lengo la kuwasidia wakulima
wadogo kuwa na uwezo wa kuongeza thamani ya uzalishaji katika wilaya ya
kilombero alisema kuwa hali ya wakulima kugoma kuchukuwa mkopo mwaka huu
kumeathili zoezi la kufanya tathimini sahihi ya mchele iliyopo wilayani
humo kupitia maghala yaliyopo maeneo yao ,pia wakulima wameshindwa kufanya
biashara ya pamoja.
Afisa mikopo kutoka benki ya{ NMB) wilaya ya kilombero Saraha Kalokola
,amesema kuwa mfumo wa stakabadhi za maghala ni mfumo unaotumika nchini
kwa kutumia bidhaa zilizohifadhiwa kwenye maghala badala ya mali
zisizohamishika kuwa dhamana ya kupata mikopo kutoka asasi za fedha na
kwamba,riba hupanda na kushuka kutegemeana na bodi yenye dhamana ya mikopo.
Kilio cha wakulima pamoja na hayo wakulima wilaya ya kilombero mkoani
morogoro wameililia serikali kukomesha tabia za wafanyara kujipangia bei za
mavuno yao pindi wauzapo mazao hayo.
wamesema tabia hizo zimekua zikiwadidimiza kiuchumi kutokana na tabia za
wafanyabia hao kuwaibia asilimia 48 ya mavuno yao pindi wauzapo mazao hayo.
Henry Risanga , Afisa kilimo kutoka taasisi ya maendeleo mjini na
vijijini [RUDI]asasiisiyokuwa ya kiserikali inayofanya kazi kwa madhumuni
ya kutoa mafunzo mbali mbali kwa wakulima yanayolenga kuongeza tija na
ongezeko la thamani ya mazao hususani zao la mpunga, ingawa juhudi zote
hizo zimegonga mwamba kutokana na wafanyabiashara kutumia mwanya wa sheria
zisizo na makali za mauzo kuwa nyanyasa wakulima kwa kuwapangia bei wanazo
zitaka wao.
“ serikali haina budi kukomesha tabia hizi ili kuwasaidia wakulima
kunufaika na kilimo hicho ili kujikwamua na uduni wa maisha”.ameongeza
Risanga.
Wakulima wameitaka serikali kuboresha mazingira ya kibiashara ilikuikuza
sekta ya kilimo hapa nchini kama ilivyokusudia kupitia sera ya kilimo
kwanza ya mwaka 208.
Mkuu wa wilaya ya kilombero Hassani Masala, amekirikuwepo kwa hali hiyo na
kusema kuwa uchangiwa na wakulima wenyewe ambao wanakataa kuifadhi mazao
kwa pamoja kwenye maghara ya selikari na kutojuinga na vyama vya ushirika
ambavyo kazi yake nikuwasaidia katika kupata masoko yanye bei zenye unafuu.
Masala ,ameongerea suala la soko huria kuwa lichangia wakulima kupangiwa
bei na wafanyabiashara na elimu dhidi ya matumizi mabaya ya mitandao ya
jamii katika kufanikisha soko.
Kimsingi wakulima wa zao la mpunga wameilalamikia Serikali kupitia wizara
ya kilimo na chakula na ushirika hapa chini kwa kushindwa kutoa elimu ya
kilimo biashara kwa wakulima ili kusaidia kupata faida itakayowasaidia
kuendeleza maisha yao pamoja na kukuza pato la taifa.
Wanasema wataalamu wa kilimo na maafisa wa biashara wanashindwa kutoa
elimu kuhusu uzalishaji wa kilimo cha mpunga ili kuendana na soko na kukuza
uchumi wa wakulima na Taifa kwa ujumla.
Wanasema kutokana na asilimia 70 ya wakulima kukosa elimu juu ya
uzalishaji wa zao hili, kumesababisha asilimia 30.1 za mazao kutokuwa na
ubora pamoja na kupata hasara asilimia 33.3 ukilinganisha asilimia 95
za gharama wanazozitumia katika uzalishaji wa kilimo cha mpunga chenye
ekari moja.
Akizungumza kwa niaba ya wakulima hao Giriadi Katengu mkulima wa mpunga
kutoka katika kijiji cha Mwaya anasema kuwa changamoto kubwa inayowafanya
kukata tamaa na kilimo
Keisi.h. ncheyo mkulima anasema kuwa ,kwa mwaka huu alifanikiwa kulima
ekali 6 za mpunga kwa gharama ya shilingi milioni 3 na laki 2 nakupata
hasara ya shilingi laki 4 kutokana na sababu kubwa ya mabadiliko ya hali ya
hewa,mbolea ambayo siyo ya kisasa pamoja na hali ya soko kuwa chini.
Mratibu wa asasi isiyokuwa ya kiserikali ya (RUDI), kata ya Mangura wilaya
ya kilombero mkoani Morogoro,Ibrahim Mghonu shirika ambalo
linajishughulisha na kutoa elimu ,kuwatafutia soko wakulima na kuandaa
vikundi kwa wafanyakazi wa mjini na vijijini,amesema Tanzania inategemea
uchumi wake kutoka katika kilimo,huku akishangazwa na serikali kupuuza
sekta hiyo muhimu.
Afisa kilimo wa halmashauri ya wilaya hiyo Malia Lesharo alikiri kuwepo
kwa matatizo hayo na kusema kuwa mbali nakuwepo changamoto hizo , idara
ya kilimo uwanawatembela wakulima kwa mwaka mara nne ambapo anasema kata
na vijiji wapo pia maafisa kilimo na maafisa ushirika.
mwisho