DAR-ES-SALAAM, Tanzania
TAMASHA la Mitindo la Dar es salaam (DFF) kwa mwaka wa pili mfululizo
linandaa tamasha kubwa la mavazi ambalo pia litahusisha mauzo ya
kawaida na ya hisani.
Tamasha hilo limetengenezwa mahususi kwa ajili ya kuwapa muda mzuri
familia kusherehekea sikukuu ya Iddi.
Katika tamasha hilo watu watapata nafasi ya kuona vivutio mbalimbali,
kula na kununua bidhaa za mavazi huku wakichangia maendeleo ya
upatikanaji wa madawati kwa wanafunzi.
Tamasha hili ambalo litahusisha wabunifu wa mavazi na wauzaji wa hapa
nchini ,litafanyika Iddi Mosi na Iddi Pili katika viwanja vya TTCL
Kijitonyama na linakadiriwa litakusanya zaidi ya watu 2000.
“Familia ndio kiini cha sikukuu ya Iddi na tamasha la Mitindo la Dar
es salaam linatoa nafasi kwa familia kutoka kwa pamoja kusherehekea
sikukuu. Tunatarajia kuziona familia zikifika hapa na kufurahia Iddi
pamoja”, alisema Bi. Lucy Naivasha, mmoja wa waanzilishi wa DFF.
Pamoja na kuwa tamasha la mitindo, DFF, inakutanisha makundi ya
wanawake wanaoshughulikia mitindo na mauzo kwa lengo la kuimarisha
biashara zao za mavazi na mitindo.
“Tamasha la mitindo linawakilisha zaidi ya mavazi, tunajaribu
kutengeneza uwanja mpana ambapo wajasirimali wanawake wanakutana,
kuzungumza na kutafuta njia ya kuimarisha ushiriki wao katika tasnia
ya mitindo.Tunaamini kwa kufanya hivyo tutakuwa tunawawezesha wanawake
kujiimarisha katika jamii”, anasema Bi. Tina Lasway,mwanzilishi
mwingine wa DFF.
Tamasha hilo la mitindo litafanyika kwa kusimamia nguzo zote tatu za
kuanzishwa kwake yaani kuanzisha mtandao, kujifunza na kuuza.
Ili kufanikisha zaidi Taasisi ya maendeleo ya wanawake katika biashara
(The Women Empowered in Business Summit –WEBS-), kwa kushirikiana na
Kituo cha Ujasiriamali cha Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kitatoa elimu
kwa wanawake kuhusu misingi ya biashara hasa kwa wanawake wanaofanya
biashara za nguo.
Aidha tamasha linatumika kama sehemu ya kutambulisha wabunifu wanawake
wapya na pia kutambulisha bidhaa zao .
“Ujasiriamali upo kwenye damu za wanawake, wote tunafanya kwa njia
moja au nyingine, lakini tunahimizwa kuifanya kwa namna bora,
tunapashwa kuondoka katika maduka na mauzo madogo hadi maduka makubwa
na mauzo makubwa” aliongeza Bi. Lasway.
Tukio la kwanza katika tamasha hilo litakuwa ni kuonesha Thamani ya
Wanawake ambapo wabunifu wapya 10 watakuwapo.
Tukio hilo litahusisha Martin Kadinda, FT EasyWear, Kali Elegance,
Zuri, Maasai Wear and Prisar.
Mustafa Hassanali, mbunifu maarufu wa Ukanda wa Afrika pia atakuwapo
kuonesha baadhi ya kazi zake kama mmojawapo wa mzizi wa masuala ya
mitindo nchini Tanzania.
Mwaka jana wabunifu sita walikuwa akiwemo Eskado Bird and Eve
Collections, Kilechia Fashion and Designs, PICHINI, Francoo, na Rio
Paul.
“Imekuwa raha tupu kuketi vitini na kuangalia jinsi wabunifu hao
wanavyokua.Tunajivunia uwapo wao” alisema Bi Naivasha.
Pamoja na kunyanyua masuala ya mitindo katika ngazi nyingine, DFF pia
inatoa namna mpya kabisa ya matunda ya ubunifu wa mitindo.Kwa mujibu
wa Bi Lasway, DFF imeungana na taasisi ya Hassan Maajar Trust (HMT)
kusaidia kampeni ya wanafunzi kupata madawati.
“Ushirikiano wetu na HMT ni wa asili kwa kuzingatia dhima zetu, kwanza
kujiwezesha na kisha kuwaambukiza wengine uwezo huo,” alisema Bi
Lasway.
Masuala mawili yatafanyika katika tamasha ili kufanikisha dhima nzima,
kwanza ni mnada na pili biashara kwa mfumo wa hisani.
Mnada utafanyika kwenye tukio la Thamani ya Mwanamke (Women’s Worth)
ambapo wabunifu wa Tanzania 12 wamejitolea vitu vyao mbalimbali kwa
ajili ya mnada.
Miongoni mwa waliowezesha mnada huo ni Kiki’s Fashion, Eve
Collections, Ally Rhemtulla, PICHINI, Joy Dar fire Arts, Francoo, FT
EasyWear na Mustafa Hassanali.
“Wakati DFF iliponiomba kuwezesha nilifurahi sana.Ama hakika nimetoa
kitu cha thamani kubwa sana kwangu. Ni vyema na haki kufanya hivyo”
alisema Ally Rhemtulla.
Biashara kwa hisani ambayo inajulikana kama duka lenye sababu njema
itafanyika wakati wa manununuzi na lengo ni kuongeza vitu ambavyo HMT
itaweza kuvitumia kuuza katika maduka yake ya hisani.
Watu watakaofika katika tamasha wanaombwa kuleta na vitu vyao ambavyo
wanaweza kuvitoa kwa ajili ya hisani kama nguo, vifaa vya ndani,
viatu nadhalika.
Watakaoleta vifaa watapewa vocha ambazo wanaweza kuzitumia kupata
nafuu katika manunuzi kwenye tamasha la mitindo.
“Wengi wetu tuna ziada katika masanduku yetu, vitu ambavyo
hatuvitumii tena.Hizi ziada ukituletea unaweza kuwezesha mabadiliko
makubwa kwa kuwezesha kupatikana kw amadawati kwa shule zinazohitaji.
Watu wanasema ukarimu huanzia nyumbani na sisi watu wa DFF2012
tunachukua nafasi hii kuleta mabadiliko” anasema Bi Zena Maajar
Mtenga, Mkurugenzi Mtendaji wa HMT.
Tamasha hilo linadhaminiwa na CRDB, Times Fm, Clouds Entertainment,
Hugo Domingo, Bongo Live, A1 Outdoor, Identity, Business Times
Limited, Events TZ, Michuzi Blog na pia fedha kutoka kwa waratibu
wenyewe.
Mawasiliano: P.O Box 2389 Dar-es-salaam, Tanzania
Simu: +255 786 499944 | Barua pepe:
info@darfashionfestival.com
|tovuti: www.darfashionfestival.com
***************************************************
Kwa wahariri
Tamasha la Mitindo la Dar es Salaam (Dar Fashion Festival – “DFF”-)
ni kampuni inayomilikiwa na wanawake na kusajiliwa nchini.
Kampuni hii inatafuta njia ya kuwezesha wanawake kushamiri katika
masuala ya biashara hasa tasnia ya mitindo kwa kuwatambua, kuwasaidia
na kuboresha masuala yao ya kibiashara.
Tasnia ya mitindo ni pamoja na mavazi,bidhaa ambatana nazo,viatu,
sanaa, samani,upambaji wa ndani na mapambo.
DFF imejipanga kuimarisha shughuli hizo kwa kuzingatia nguzo tatu
ambaoz ni kutengeneza Mtandao, Kujifunza na kuwezesha mauzo.
DFF inawapatia wanawake eneo la kukutania, elimu inayostahili na
raslimali za kuwezesha kusonga mbele kutoka katika fungu dogo hadi
kujitosheleza na kuwa imara ; pia kuwezesha kuwa na tasnia ya mitondo
katika sekta binafsi inayokua kwa kasi.
DFF imejipanga kuwezesha ndoto za wanawake zinatimia.
www.darfashionfestival.com
The Hassan Maajar Trust ni taasisi isiyo ya kiserikali isiyojihusisha
na kibiashara, kidini wala faida ambayo hufanyakazi na watu wa aina
zote Tanzania na duniani kwa lengo la kuboresha mazingira ya kusomea
ya wanafunzi wa Tanzania kwa kuwapatia madawati na vifaa vingine vya
masomo.
Taasisi hiyo imeanzishwa kwa kumbukumbu ya Hassan Shariff Maajar
(Hashy) ambaye alikufa akiwa na miaka 18 katika ajali ya gari Novemba
11, 2006.
Hassan alikuwa mwanafunzi wa Waterford Kamhlaba United World College
of Southern Africa mjini Mbabane, Swaziland.
Kwa sasa tunakusanya fedha kwa ajili ya madawati kwa shule za msingi
za Tanzania.
Kutokana na takwimu zilizopo kutoka Wizara ya elimu na mafunzo ya
ufundi kuna, uhaba wa madawati milioni 3.0 nchini. Na mipango ya
taasisi ni katika miaka mitatu kuwezesha kuwapo kwa madawati ya
kutosha kila mwanafunzi. Kampeni yetu ni: “Ni dawati kwa kila
mwanafunzi Child”. www.hassanmaajartrust.org