Wakausha uke kuvutia mapenzi

 

 

NCHINI Zambia kuna imani kwamba uke mkavu unaonesha  uaminifu wa mwanamke katika maisha  yake ya kike. Kutokana na hali hiyo wanawake wengi wamekuwa wakitumia mizizi kuondoa ute unaolainisha njia hiyo, ama kw akuingiza dawa hizo au kuzinywa.

Pamoja  maamuzi hayo ambayo ni ya kibinfsui mno madaktari nchini hapa wamesema kwamba  utamaduni huo unaoshika kasi una hataraisha maihs aya wanawake kwani mizizi mingine ni hatari kwa maisha yao.

Dora, 39, amekaa katika ndoa yake kwa miaka 18 sasa. Anasema kwamba kudumu kwa ndoa yake kunatokana na matumizi ya mizizi ambayo  hufanya uke wake kuwa mkavu.

Anasema uke wenye uchevunyevu hutoa ishara mbaya kwa mume.

“Kama uke wako una unyevunyevu , mwanaume anaweza kufikiria kwamba wewe una vitabia vya umalaya na hivyo atakuacha na kwenda kwa mwanamke mwingine,” anasema Dora.

Dora anasema kwamba alijifunza masuala ya kuufanya uke kuwa mkavu wakati wa mafundisho ya ndoa yao iliyofungwa kimila, na tangu wakati huo mume wake hajawahi kunung’unika kuhusu chakula cha usiku.

“Najua namna ya kujiweka sawa mwenyewe,” anasema Dora, ambaye alitafadhalisha kutumiwa kwa jina lake la kwanza pekee katika utambulisho kwenye mahojiano.

Wanawake katika ukanda huu wa Afrika wamekuwa wakitumia mizizi kuzuia  unyevunyevu wa uke, wakisema kwamba kitendo hicho hufanya mapatna wao waridhike sana katika kitendo cha kungonoana.

Unawezaje kufurahia kufanya mapenzi wakati husikii kuta za mwenzako? Anauliza Luka banda ambaye anafurahishwa na kitendo hicho cha kukausha uke.

Wakati ni utamaduni kwa wanawake kujichomeka mizizi katika maeneo yao ya uke, wataalamu wa masuala ya dawa na tiba wa kisasa wanasema tabia hiyo inakaribisha  madhara makubwa kama kujichubua na hata kusababisha vidonda wakati wa msuguano wa via vya uzazi wakati wa kufanya mapenzi.

Na michubuko pamoja na vidonda ni moja ya njia  za kuambukizana  ugonjwa wa ukimwi na magonjwa mengine.

Kwa sasa wanawake wengi wanakula dawa hizo kupitia unga uliosagwa wa mizizi unaochanganywa katika uji au chakula kingine. Hii inasaidia kutosababisha michubukona vidonda katika uke.

Dora, ambaye alishawahi kufanya utumbukizaji wa mizizi pamoja na vidonge vya chumvi katika uke wake anasema kwamba unga wa mizizi unaochanganywa na uji ubnafanya kazi nzuri zaidi.

Wataalamu wanasema kwamba  ukaushaji wa uke nchini Zambia ni tabia iliyo ndani ya makabila manegi na wanawake wengi ingawa hakuna takwimu sahihi kuhusiana na hilo.

Theluthi mbili ya wanawake 812 wa Zambia waliohojiwa katika utafiti wa saikolojia, afya na tiba uliochapishwa 2009 walisema kwmaba wametumia mizizi ya asili kufanya uke uwe mkavu wakati wa kufanya mapenzi.

Nusu yake walisema wanaendelea kutumia.

Suala la ukaushaji wa uke pia umeshawahi kuripotiwa pia nchini Afrika Kusini DRC na Zimbabwe.

Wauzaji wa mizizi hiyo wamesema kwamba wanawake wengi hufurahia kula dawa hizo kwa kuchanganya na  uji.

“Bidhaa tunazouza hapa nyingi ni zile za kutumia kwenye uji au katika maji ya moto,” anasema Josephine Munsaka, ambaye anauza dawa za kukauka uke. “Ni nadra sana kupata mwanamke anayetaka mzizi wa kuingiza katika uke, labda mmoja katika kila watu 20.”

Josephine Munsaka anauza mizizi hiyo katika soko la Mtendere mjini Lusaka. Mizizi yake ni pamoja na iliyosagwa inayoweza kunyweka na inachangia kukausha uke.

Utumiaji wa mizizi hiyo unatokana na  imani kwamba uke wa mwanake unaweza kujaa maji au kupwerepweta kama ishara ya kuwa na mahawara wengi.

“Kitabibu hakuna kitu kwenye uke kinaitwa kupwerepweta au iliyojaa maji,” anasema Dk Lottie Hachaambwa, mtaalamu wa magonjwa ya kuambukiza katika hospitali ya mafunzo ya Lusaka.

“Ute katika uke unasaidia kulainisha njia wakati wa kufanya mapenzi nah ii ni kawaida.”

Ingawa inajulikana kwamba ukaushaji wa uke ndio njia nzuri kwa kuwa inasaidia kuta za uke  kujaa, mwanamke akicha kutumia anaweza kupata maambukizi yanayosababsihwa na  tiba hiyo na inaweza kusababisha utokaji wa uchafu usiokuwa wa kawaida

Kauli hiyo ya Dk Hachaambwa inasema kwamba kutokana na hali hiyo mwanamke anaweza kulazimika kurejea kutumia mizizi hiyo.

Wanawake ambaow anajikuta wanatokwa na uchafu usiokuwa wa kawaida unatokana na  kuwa na fangasi, magonjwa ya kuambukiza ya ngonoi na hata bacteria.

Pia amesema kwamba kwa kutumia mizizi inachosokomezwa katika uke kuna hatari ya kupata maambukizi ya ukimwi.

“Ufanyaji mapenzi katika uke mkavu kunaweza kuongeza nafasi ya kuambukizana ugonjwa ukimwi kutoka na na msuguano katika kuta za uke.,”  anasema Hachaambwa na kuongeza kwamba kama kukiwepo na michubuko virusi vya ukimwi vinaingia katika mkondo wa damu kirahisi mno.

Aidha imeelezwa kuwa kondomu inaweza kuchanika kama haitasaidiwa na unyenyevu wa kutosha katika uke.

Lakini wanawake wengi haopa wanasema uke mkavu  ni kitu muhimu katika kuwa na mahusiano ya kudumu ya mapenzi na mtu wako.

 

WhatsApp Image 2018-12-02 at 11.28.51

Chanzo: Global Press