JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIAWIZARA YA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIATANGAZO LA USITISHWAJI WA MATANGAZO YA TELEVISHENI KWA KUTUMIATEKNOLOJIA YA ANALOJIA NA KUHAMIA TEKNOLOJIA YAUTANGAZAJI YA DIJITALI: Nchi yetu itasitisha rasmi matumizi ya teknolojia ya utangazaji ya analojia na kuhamiateknolojia ya dijitali ifikapo tarehe 31 Desemba, 2012 saa sita usiku.Lengo la kufanya hivyo ni kuendana na kasi ya ukuaji wa teknolojia ya mawasiliano dunianikote. Miongoni mwa faida za kutumia teknolojia ya dijitali ni kuongezeka kwa ubora wamatangazo ya televisheni, ongezeko la chaneli za televisheni litakalotokana na matumizibora ya masafa, kuwepo kwa masafa ya ziada yatakayopatikana baada ya kuzimwa kwamitambo ya analojia inayotumia masafa mengi, kuongezeka kwa watoa huduma wamawasiliano ya simu, matangazo ya televisheni kupatikana katika vifaa vingi zaidi vyamawasiliano kama vile simu za mkononi na kompyuta kupitia mtandao wa intaneti.Hivyo, nachukua fursa hii kuwajulisha na kuwahimiza wananchi wote kufanya maandaliziya kukabiliana na mabadiliko hayo kwa kutumia ving’amuzi vitakavyowezesha televisheniza analojia zinazotumika kwa sasa kupokea matangazo ya dijitali au kutumia televisheni zadijitali ambazo hupokea matangazo ya digitali moja kwa moja.Kwa taarifa zaidi piga simu namba 0784 558 271 au tembelea tovuti zifuatazo:wwww.mst.go.tz au www.tcra.go.tz