NA MAGRETH KINABO- MAELEZO : WATU zaidi ya 500, 000 wanatarajiwa
kunufaika baada ya Kampuni ya Bia ya Serengeti (SLB) kutenga zaidi
ya sh.milioni 300 kwa ajili ya miradi salama ya maji na usafi
kwenye mikoa minne nchini .
Hayo yalisemwa leo(jana) na Meneja wa Uhusiano na Mawasiliano kwa
kampuni hiyo, Teddy Mapunda wakati akizungumza na waandishi wa habari
kuhusu
maadhimisho ya wiki ya maji yatakayofanyika kitaifa mkoani Iringa
kuanzia Machi 16 hadi 22,mwaka huu.
Alisema kati ya fedha hizo sh. milioni mbili zitatumika katika miradi
ya maji kwenye mikoa ya Mwanza, Kilimanjaro, Dares Salaam na Iringa.
Aliongeza
kuwa katika mkoa wa Iringa fedha hizo zitatumika kuzindua mradi wa
uvunaji wa maji na uboreshaji wa miundombinu maeneo ya hospitali,
wakati sh. milioni
moja kudhamini vipeperushi na vijarida.
“Tunawekeza fedha hizo mahali ambapo tuna viwanda kwa sababu tukitumia maji
inabidi tuyarudishe,” alisema Teddy.
Teddy alifafanua kuwa SBL inafanya kazi kupunguza matumizi ya maji katika
vifaa vya uzalishaji na mfululizo wa toaji wa bidhaa zao, ambapo inahusisha
uboreshaji madhubuti wa maji katika mitambo yao, kuhakikisha matumizi ya
maji katika maeneo yanazingatiwa na kupunguza majitaka.
Aliongeza kuwa wamekusuia kuongeza njia za upatikanaji wa maji kwenye jamii
zinayowazunguka na usimamizi wa vyanzo vya maji.
Naye Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maji Vijijini, Amani Mafuru alisema
maadhimisho hayo yatafanyika kwenye uwanja wa Samora, hivyo aliwataka
wannachui wajitokeze ili kuweza kushiriki , kutoa tathimini na kuishauri
serikali kuhusu sekta hiyo.
Tatizo la maji limekuwa likiathiri kila bara duniani na zaidi ya asilimia 40
ya watu.
Hadi kufikia mwaka 2025 watu bilioni 1.8 watakuwa wanaishi katika ama mikoa
ambayo haina majisafi kabisa , na theluthi mbili ya idadi ya watu duniani
inawezekana wanaishi katika hali ngumu ya upatikanaji wa maji.
Mwisho.