Kama sehemu ya Maadhimisho ya mika 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara,
wanahabari 10 wanapanda Mlima Kilimanjaro kwa mwaliko wa Hifadhi za
Taifa (TANAPA).
Jana (Jumanne) wanahabari hao ambao wako chini ya uongozi wa Pascal
Shelutete ambaye ni Meneja Uhusiano wa TANAPA, walifanikiwa kufika
katika kituo cha pili cha kupanda Mlima huo kiitwacho Horombo.
Wanahabari hao wanategemea kufika kileleni mapema tarehe 9/12/2011
kama ilivyopangwa. Wanahabari hao wanapanda mlima huo wakiwa pamoja na
kikundi cha wanajeshi ambacho kinaupandisha Mwenge wa Uhuru Mlimani
Kilimanjaro.
Wanahabari hao ni Asraji Mvungi wa ITV, Daniel Mjema wa Citizen, Musa
Juma wa Mwananchi, Emmanuel Amasi wa TBC na James Range wa Star TV.
Wengine ni Irene Mark wa Tanzania Daima, Lilian Joel wa Uhuru, Salome
Kitomari wa Kilimanjaro Press Club, Juma Kapipi wa Channel Ten,
Nicholaus Mbaga wa TBC na Sheiba Bulu wa Wizara ya Maliasili na
Utalii.
George Matiko
MSEMAJI WA WIZARA
7/12/2011