Airtel KUKUZA MAWASILIANO NYANDA ZA KUSINI

*
*

**· **Mawasiliano ya Airtel kusaidia kukuza utalii mbuga za KITULO
wilayani Rungwe.****

**· **Yafikisha huduma za mawasiliano katika vijiji 20 ndani ya
mwezi mmoja mikoa ya Rukwa, Iringa, na Mbeya,**

*Tarehe 22, 2011* Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imeendelea
kuwafikishia wakazi wa nyanda za kusini huduma za mawasiliano bora na kwa
bei nafuu.****

Airtel imefikisha huduma za mawasiliano katika vijiji vipatavyo 20 ndani ya
mwezi mmoja vyenye idadi ya watu wapatao 52,775 ambao kwa kupitia mtandao wa
Airtel wataweza kuboresha shughuli za kilimo , biashara, katika kuinua
uchumi wa jamii na nchi kwa ujumla.****

Vvijiji vitakavyofaidika na huduma hizi ni Kaulolo, Nsenkwa,Mtakuja,Inyonga
na Kamsisi mkoani Rukwa kwa Mkoa wa mbeya ni vijiji vya
OldVwawa,Isangu,Ilolo,Ilembo,Mwantengo,Hasamba,Ukingani Majengo,
Mpangala,Kinyika,Ndapo,Nhungu,Matamba na Mahanji wakati Mkoani Iringa ni
Kibena, Tea estate ****

Akiongea kwa niaba ya kampuni ya simu za mkononi ya Airtel Meneja Uhusiano
wa kampuni ya simu ya Airtel Jackson Mmbando alisema” Mawasiliano ni muhimu
katika kuboresha ulinzi, kukuza uchumi, kuweka jamii pamoja na kwa kutambua
hilo, Airtel tumewekeza zaidi katika kupanua huduma zetu za mawasiliano hasa
vijijini ambapo ndiko kwenye changamoto kubwa”.****

Airtel tumeweza kuwafikishia huduma za mawasiliano kwa Wakazi wa maeneo ya
Matamba eneo maarufu kwa shughuli za kilimo na utalii, Pia tumewekeza
kikamilifu na sasa mawasiliano bora yanapatika katika mbuga za KITULO
zilizoko wilayani Rungwe mkoani Mbeya, wataliii sasa wataweza kuwasiliana na
ndugu zao wakiwa katika ziara ya mbuga hizo aliongeza Mmbando****

** **

Airtel inaendelea kupanua mtandao wake na kuwapatia wateja wake huduma bora
na kwa bei nafuu zinazopatikana nchni nzima, lengo likiwa ni katikati
kutimiza dhamira yake katika kuwafikia wananchi wengi na kuboresha huduma za
mawasiliano nchini hasa katika vijiji mbalimbali nchini****

** **

“Mkakati wetu wa kupanua mawasiliano vijijini unaendelea kwa kipindi chote
cha Mwaka huu lengo letu ni kuhakikisha tunawafikishia wananchi wote huduma
ya mawasiliano yenye utulivu zaidi na kutatoa uhuru wa mawasiliano zaidi
kwa wateja kuendelea kufanya mawasiliano yenye manufaa yatakaowafanya
wafurahie kutimiza miaka 50 ya uhuru wakiwa na miundombinu ya mwasiliano
yanayojitosheleza” alimaliza kusemba Mmbando****

** **

Mwisho****

** **