*
HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI WIZARA YA ARDHI NYUMBA
NA MAENDELEO YA MAKAZI MHE. HALIMA JAMES MDEE (MB) KUHUSU MAPITIO YA
UTEKELEZAJI WA BAJETI YA MWAKA 2010/2011 NA MAKADIRIO YA MATUMIZI YA WIZARA
YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI MWAKA WA FEDHA 2011/2012**
*
*
UTANGULIZI**
Mheshimiwa Spika* , napenda kuchukua nafasi hii kumshukuru Mwenyezi Mungu
kwa kuniwezesha kuwepo hapa leo kuwasilisha maoni ya Kambi ya upinzani
kuhusu Wizara ya Ardhi, Nyumba Na Maendeleo ya Makazi.*
Mheshimiwa Spika*, pia nikushukuru wewe kwa kuniruhusu kutoa maoni ya Kambi
ya Upinzani kuhusu Wizara hii kwa mujibu wa Kanuni ya 99 kanuni ndogo ya (7)
, ya Kanuni za Bunge Toleo la Mwaka 2007.*
Mheshimiwa Spika,* pili ningependa kutoa shukrani zangu za dhati kwa Chama
Cha Demokrasia na Maendeleo *(CHADEMA)* na wananchi wa Jimbo la Kawe kwa
imani yao kwangu, Makamanda wote (vijana, wazee na akina mama wa vyama
vyote) walioshiriki katika harakati zote za Kampeni na hatimaye kukesha na
mgombea wao, Shule ya Msingi Oysterbay kulinda ushindi wetu. Mungu pekee
ndiye anayejua shukrani yangu kwao! Ahadi yangu kwao, ni kuwatumikia kwa
uwezo wangu wote kwa kadiri Mwenyezi Mungu atakavyoniwezesha!*
Mheshimiwa Spika,* napenda pia kutoa shukrani za dhati kwa aliyekuwa mgombea
Urais kupitia CHADEMA, Dkt. Wilbroad Peter Slaa. Hakika wabunge wengi
tuliofanikiwa kushinda, sehemu ya ushindi ilipatikana kutokana na utumishi
wake uliotukuka katika Taifa hili! Mungu akupe uhai,naamini ipo siku
tutaifikia Nchi ya Ahadi!*
Mheshimiwa Spika,* sina budi kumshukuru Kiongozi wa Kambi ya Upinzani, Mhe.
Freemani Aikaeli Mbowe, kwa kuniamini na kuniteua kuwa Msemaji Mkuu wa kambi
ya Upinzani katika Wizara hii. Shukrani pia ziende kwa wasaidizi wa Kiongozi
wa Kambi, Kabwe Zitto (Naibu Kiongozi wa Kambi) na Tundu Lissu (Mnadhimu wa
Kambi) kwa kutuongoza vyema katika shughuli hii ngumu ya kuwatetea wanyonge.
Shukrani pia ziwafikie wabunge wenzangu wote wa Kambi kwa ushirikiano wao
kwangu.*
Mheshimiwa Spika, *sina budi pia kuishukuru sana familia yangu yote,wazazi
wangu Prof. James Salehe Mdee na Theresia Kisenga Ngowi kwa upendo wao na
kwa upekee nimshukuru kaka yangu Joseph James Mdee, ambaye alikuwa sambaba
na mimi, na timu yangu ya kampeni iliyoongozwa na uongozi wa Jimbo la Kawe
usiku na mchana mpaka kikaeleweka!*
Mheshimiwa Spika,* mwisho lakini kwa umuhimu mkubwa, napenda kutoa shukrani
zangu za dhati kabisa kwa kaka yangu na rafiki yangu mkubwa Mhe. Zitto
Zuberi Kabwe, Mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini. Kwa yeyote anayemuona
Halima Mdee,na mafanikio yake, afahamu kwamba safari yangu ya mafanikio ya
kisiasa yalianzia mbali sana! Na katika safari hii, tokea hatua za awali
kabisa, kaka yangu huyu alikuwa mhimili mkubwa. Asante sana.*
Mheshimiwa Spika*, ardhi ya Tanzania ina ukubwa wa kilomita za mraba 942,600
sawa na hekta milioni 94.26, kati yake kilomita za mraba 888,200 sawa na
hekta milioni 88.82 ni eneo la nchi kavu. Ili ardhi hii iwe na maana katika
kuleta maendeleo ni lazima kila kipande kitambiliwe kupimwe, kimilikishwe na
kupangiwe matumizi, lakini hadi sasa ardhi iliyopimwa na kumilikishwa
inakadiriwa kuwa ni asilimia moja tu. Jambo hili ndilo limepelekea migogoro
isiyoisha baina ya watumiaji mbalimbali wa ardhi. Aidha, Serikali kwa
makusudi wanapindisha matumizi ya ardhi kwa kuwamilikisha viongozi wa nchi
na wafanyabiashara wakubwa kama itakavyojionyesha katika hotuba hii.
*Mheshimiwa Spika,* asilimia hii finyu ya utambuzi wa ardhi haina maana kuwa
ardhi iliyobaki haitumiki au haina mwenyewe, kwani wananchi kwa miaka mingi
wamekuwa wakiitumia katika kuendesha maisha yao, hivyo utaratibu wowote
unaofanywa na Serikali kuimilikisha kwa mtu yoyote bila kwanza kuhusisha
wale watumizi wa awali ni chanzo na kichocheo cha migogoro. Hivyo ardhi
iskikodishwe kabla ya kuwafikiria watumiaji wa ardhi hiyo kwenye maeneo
husika (wakulima na wafugaji).
*MAMLAKA YA USIMAMIZI WA ARDHI*
*Mheshimiwa Spika, *Wizara ya ardhi ni wizara mtambuka, chini ya Taasisi
yake ya Tume ya Taifa ya Mipango wizara ina wajibu wa kuratibu utayarishaji
na utekelezaji wa mipango na matumizi ya ardhi ikiwa ni pamoja na kutenga
maeneo ya uwekezaji, kilimo (ikiwa ni pamoja na kusaidia kupatikana kwa kwa
ardhi kwa ajili ya utekelezaji wa Kilimo kwanza), makazi, malisho (ufugaji),
wanyamapori, misitu, vyanzo vya maji na shughuli zote zinazotumia ardhi.
*
Mheshimiwa Spika,* Ardhi ndio nchi, Ardhi ndio msingi wa maendeleo. Kwa hiyo
hakuna amani,ustawi wala maendeleo kwa wanadamu bila matumizi bora na
endelevu ya ardhi. Kwa bahati mbaya, baada ya kukumbatia sera ya uchumi
huria ambalo limegeuzwa kuwa holela, uongozi wa nchi yetu umetelekeza kabisa
wajibu wa kusimamia matumizi yenye tija ya ardhi kwa nchi yetu na watu wake.
*Mheshimiwa Spika, *kushindwa huko kumejidhihirisha katika maeneo makuu
mawili. Moja, masuala ya *usimamizi wa ardhi* yamewekwa chini ya Wizara
zaidi ya moja hivyo hivyo kuleta mkanganyiko kwenye suala la uwajibikaji.
Kuna muingiliano mkubwa sana wa majukumu baina ya Wizara ya ardhi nyumba na
maendeleo ya makazi na ofisi ya waziri Mkuu Tawala za Mikoa na serikali za
Mitaa ( TAMISEMI). Pili, usimamizi wa maafisa za ngazi za kati na za juu
umedhoofika kwa sababu ya kuwajibika kwa zaidi ya mamlaka moja. Mfano halisi
ni maafisa ardhi wa halmashauri ya miji na wilaya ambao wanategemewa kuwa
chini ya wakurugenzi wa halmashauri na wakati huo huo kuwajibika kwa
Kamishna wa Ardhi na Waziri wa Ardhi. Hali hii imesababisha kuongezeka kwa
migogoro ya ardhi kutokana na kukosekana kwa usimamizi thabiti wa Maafisa
Ardhi.*
Mheshimiwa Spika*, takwimu za Serikali zinaonyesha kuwa halmashauri za
wilaya zinaupungufu mkubwa wa wataalam wa ardhi kwa asilimia 74, ikiwa ni
sababu mojawapo ya kukua kwa kasi ya ajabu kwa vyombo visivyo na mamlaka
kisheria kushiriki katika usimamizi, utawala na kutengeneza matumizi bora ya
ardhi ya vijiji kama vile mkuu wa wilaya, mbunge, kamati za ulinzi na
usalama na mkuu wa mkoa. Kwa mujibu wa sheria za ardhi namba 4 na 5 za mwaka
1999 na ile ya serikali za mitaa namba 7 ya mwaka 1982, hawa hawahusiki na
usimamizi wa ardhi za vijiji.*
Kambi ya Upinzani* inaitaka Serikali kueleza mkakati ilionao wa kuviimarisha
vyuo vya ardhi vya Tabora na Morogoro ili viweze kutoa wahitimu wengi ili
kupambana na upungufu uliopo?
*Mheshimiwa Spika, *Kutokana na kila taasisi/idara/wizara kujifanyia mambo
yake, tumeshuhudia kutupiana mpira baina ya Wizara ya Ardhi, Wizara ya
Maliasili na Utalii, Ofisi ya Waziri Mkuu *(TAMISEMI)* na Wizara ya Nishati
na Madini juu ya mgogoro wa ardhi unaowahusisha *wakulima wa kijiji cha
Nzasa* wakipinga kuondolewa katika makazi yao halali. Katika mgogoro huu
Wizara ya Maliasili na utalii wanataka kuwaondoa wananchi katika ardhi yao
halali kwa madai kwamba wanaishi ndani ya hifadhi ya *Msitu wa Kazimzumbwi*.
*Mheshimiwa Spika,* Hifadhi ya Msitu ya wa Kazimzumbwi ilianzishwa na Gavana
E.F Twinig kwa Tangazo la serikali Na. 306/1954 la tarehe 24/9/1954. Tangazo
hili liliweka mipaka ya Hifadhi ya Misitu wa Kazimzumbwi. Kwa mujibu wa
mipaka husika, eneo lililo katika mgogoro halimo katika hifadhi hiyo. Na
hata kama lingekuwepo, kwa mujibu wa hukumu za Mahakama utaratibu wa
kisheria wa kutangaza eneo kugeuzwa kuwa na hifadhi haukufuatwa hivyo
kubatilisha zoezi zima! *
Mheshimiwa Spika, *kufuatia malalamiko hayo Ikulu ilimwandikia barua Waziri
wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi barua yenye Kumb. Na. CEA
110/302/IV/01 ya tarehe 10/6/2008 ikitaka wizara ikapime eneo la* Nzasa-
Chanika *kujiridhisha kama kweli wakulima hao walikuwa ndani ya msitu wa
Kazimzumbwi au la. Barua ambayo haijapatiwa majibu mpaka leo.
*Mheshimiwa Spika*, Kambi ya Upinzani inaitaka Wizara, iliambie Bunge hili
tukufu ni kwa namna gani walifanyia kazi barua toka Ikulu zenye kumbukumbu
namba *CEA 110 /302/IV/01 ya tarehe 10/Juni 2008 *na barua yenye kumbukumbu
namba *CEA 110/302/IV/01 ya tarehe 18 Septemba 2009* hasa ikizingatiwa
kwamba kuna tuhuma kutoka kwa wanakijiji kwenda kuwa viongozi wa serikali ya
CCM wanatumia Idara ya Maliasili kama Gamba kutaka kunyang’anya ardhi ya
kijiji kwa manufaa yao binafsi.
*MIGOGORO YA ARDHI*
*
Mheshimiwa Spika*,migogoro ya ardhi hapa nchini hivi sasa imekithiri kufikia
hatua ya uvunjifu wa amani na kufikia hadi umwagaji damu na pengine vifo
kutokea katika maeneo kadhaa. Hali hii imeondoa utamaduni wetu wa asili wa
kuvumiliana na kumaliza matatizo yetu kwa njia mwafaka za mazungumzo. Ni
muhimu serikali ikaelewa kwamba kupuuza* migogoro hii ya ardhi nchini ni
sawa na kuatamia bomu, hivyo ni l**azima hatua za haraka zichukuliwe!
*
*UWEKEZAJI, UBINAFISHAJI NA HATMA YA ARDHI YA TANZANIA*
*Mheshimiwa Spika, *Migogoro, hasa ya wananchi na wawekezaji inakua kwa kasi
na kuchukua sura mpya. Anapokuja *‘mgeni’*, kwa jina la
*‘Mwekezaji’*matendo ya Serikali yetu, yanapingana na usemi usemao
*‘mgeni njoo mwenyeji apone*’ bali imekuwa ‘*mgeni njoo mwenyeji asulubike’*.
*Mheshimiwa Spika, *wakati Serikali inawapa matumaini makubwa wakulima wa
Tanzania , kwa mipango kabambe ya kilimo cha kisasa, pamoja na uwekezaji
mkubwa wa kilimo utakaogharimu mabilioni za dola la kimarekani kutoka kwa
wanaoitwa wafadhili, hoja za msingi ni kama kilimo hicho kina malengo ya
kumnuufaisha mkulima wa Tanzania , au malengo yake ni kupokonya ardhi ya
wazawa na kisha kuwageuza vibarua /manamba ndani ya ardhi yao!*
Mheshimiwa Spika,*Utafiti uliofanya na HakiArdhi juu ya hali ya maeneo
yaliyokuwa ya Nafco, NARCO na Mashamba yaliyotelekezwa wamebainisha
yafuatayo:
1) Ubinafsishwaji wa mashamba ulitawaliwa na utata na udanganyifu mkubwa
hali iliyopelekea uadui baina ya wawekezaji na wakulima wadogo wadogo kwa
upande mmoja na mgogoro kati ya wakulima wadogo na wafugaji kwa upande
mwingine
2) Katika maeneo ya yaliyokuwa mashamba ya Ngano, Hanang (Hanang Wheat
Complex (HWC)) na Dakawa Ranch iligundulika kwamba wakati wananchi
wanaozunguka mashamba hayo wana mahitaji makubwa sana ya ardhi wawekezaji na
vigogo wenye fedha wamejilimbikizia maeneo makubwa ambayo hawayaendelezi kwa
kwa ukamilifu[1]
Kambi ya upinzani inaitaka serikali ilieleze Bunge hili tukufu na watanzania
kwa ujumla nini kilichojiri katika ugawaji wa ardhi ya iliyokuwa Dakawa
Ranch na ni wanakijiji wangapi walinufaika na mgao huo!
*3) Wawekezaji kuwakodisha wananchi wenyeji mashamba kwa ajili ya kilimo na
kuwatoza fedha. Haya yalitokea katika Mashamba yanayomilikiwa na Rai Group
ambapo wananchi walikuwa wanakodisha $ 10 kwa ekari. Hali kama hii pia
inafanyika katika Shamba la mpunga Mbarali na Kapunga, yote yakiwa wilaya ya
Mbarali.[2]
kurejeshwa kwa wananchi lakini hayajarejeshwa , kati ya mashamba hayo ni
shamba la Gawal na Warret ,lililopo Hanang lenye ukubwa wa hekta 4,000.
Maamuzi ya kuyarejesha mashamba kwa wananchi yalifanyika toka mwaka 2004/05.
[3]
serikali kuhusiana na mustakabali wa mashamba haya! Kambi ya upinzani
inaitaka pia serikali itoe tamko juu ya mustakabali wa shamba la Bassotu.
*KIJIJI CHA CHASIMBA- BOKO – DSM*
*Mheshimiwa Spika,*Hivi karibuni kumekuwa na matamko mbali kutoka kwa
kampuni ya Saruji, (Tanzania Portland Cement Co. Ltd), ikitishia kufunga
kiwanda, kwa madai kwamba hawana eneo la kutosha . Hoja yao kubwa ni kwamba
wananchi wa kijiji cha Chasimba wamevamia eneo lao! Na kwamba wanashindwa
kujipanua kama kiwanda. *Mheshimiwa Spika,*Nimeona nilizungumze hili ili
kuondoa upotoshwaji unaotaka kufanywa na kiwanda husika. Ni muhimu bunge
hili tukufu likafahamu kwamba , Chasimba iko ndani ya ,Kijiji cha Boko,
kijiji ambacho kiliandikishwa kama kijiji kwa mujibu wa sheria ya
kuandikisha vijiji,kutambuliwa kwa Vijiji vya Ujamaa na Uongozi wa Vijiji
,1975 na hati kutolewa 25/2/1976[4]
hakuna mazingira yoyote yanayoonyesha kwamba kijiji hicho kilifutwa ama
kubatilishwa.Lakini kama ilivyo kawaida yetu, kuendekeza wawekezaji dhidi ya
wenyeji, wanakijiji waliuzwa wakiwa ndani ya ardhi yao, ndipo likaja suala
la kujalidiana kuhusu fidia! Zoezi ambazo liliendeshwa kihuni hasa
ikizingatiwa kwamba mwekezaji alikuwa na hati tayari! *Mheshimiwa Spika,*Wakati
mwekezaji akidai anamiliki eneo lote la viwanja 1,4 na 7 kuna nyaraka za
Serikali zinazoonyesha kwamba mwekezaji husika hakupewa umiliki wa eneo
lote, kuna eneo ambalo lilibaki serikalini na mchakato wa kutengeneza hati
mbili ulikuwa umefanyika na kufikia hatua za mwisho kabisa na nyaraka
zipo!*Mheshimiwa
Spika,*Hoja ya kiwanda kushindwa kujitanua kwa sababu haina eneo la kutosha
,hazina mashiko hata kidogo. Kwa mujibu wa barua kutoka kwa Mkurugenzi wa
manispaa ya Kinondoni ya tarehe 30/5/2002 kwenda kwa Mkurugenzi wa Maendeleo
ya makazi, Wizara ya ardhi na Maendeleo ya Makazi. Barua husika inaelezea
ombi ambalo manispaa ya Kinondoni ililipata kutoka kwa M/S Tanzania Portland
cement company Ltd la kutaka kugawanywa kiwanja na 1,4 & 7.*Mheshimiwa
Spika, *barua husika inabainisha kwamba kikao cha kamati ya Mipangomiji na
Mazingira kilichofanyika 22/5/2002 kililijadili suala hilo na kulikubali
kutokana na wawekezaji katika kiwanda hicho kutokuwa tayari kulipia eneo
ambalo si la uzalishaji na wala si la malighafi! Kwa ujumla eneo lote lina
ukubwa wa hekta 922.22, eneo linalohusika na uzalishaji na malighafi lina
ukubwa wa hekta 685. Eneo ambalo halitumiki na mwekezaji ni hekta236.63. Ni
eneo hili ambalo ndilo lina makazi ya wananchi ,ambao wengi wao
walidhulumiwa kwa kulazimishwa kumpisha mwekezaji! pasipo utaratibu wa
kisheria kufuatwa!*Mheshimiwa Spika, *tumekuwa tunaishauri Serikali, ambayo
inataka kuwaondoa wananchi kwa nguvu, kuliangalia hili suala kwa busara ya
hali ya juu. Tofauti na maeneo mengine ambayo kuna uvamizi wa maeneo ya
watu, wananchi eneo hili, wengi wao ni watu wazima, ambao wana kila ushahidi
wa kuonyesha kwamba pale ni asili yao na kilichofanyika ni dhuluma dhidi yao
kupisha wenye fedha. Na hawako tayari kuacha makazi yao, wakiungwa mkono na
Mbunge wao na madiwani wao wa Kata za Wazo na Bunju (CCM)! Tumeweka itikadi
pembeni!* UFISADI WA ARDHI NA MUSTAKABALI WA MTANZANIA MASIKINI*
*MKOA WA MBEYA*
*Mheshimiwa Spika*, katika wilaya ya Mbarali, shamba la Mpunga la Mbarali
(Mbarali Rice Farm- ekari 14437) na shamba la mpunga la Kapunga (ukubwa
ekari 18425) yalikuwa ndio chanzo cha mapato cha wananchi wa eneo husika.
Mashamba haya yalikuwa yanahudumia watu zaid ya 30,000 na vijiji kumi .
Ardhi hiyo pia ilikuwa inahudumia watu wa Iringa na wilaya nyingine za
Mbeya. Mipango ya awali ya Serikali , mwaka 2003/2004 kama ilivyobainishwa
na na aliyekuwa Waziri wa Kilimo ilikuwa ni kuyabinafsisha mashamba hayo kwa
wakulima wadogo wadogo, mpango ambao ungejumuisha mashamba ya Ruvu na
Dakawa.
*Mheshimiwa Spika*,Kutokana na nguvu ya mafisadi kuizidi hekma ya serikali ,
na licha ya kilio cha aliyekuwa mbunge wa Mbarali kipindi hicho , Mhe .
Esterina Kilasi , serikali iliamua kuuza eneo husika kwa kampuni ya Highland
estates Ltd . Mmiliki wa sasa Bwana Nawab Mulla ni Mwenyekiti wa Chama Cha
Mapinduzi mkoa wa Mbeya. Wananchi wamegeuka wapangaji kwa kukodisha maeneo
ili waweze kulima na kujipatia kipato!*
Mheshimiwa Spika, *wakati Shamba la Mbarali akipewa kwa bei ya kutupa
Mwenyekiti wa CCM, shamba la kapunga[5]
kampuni ya Export Co. Ltd kwa bei ya
kutupa ya shilingi bilioni 2.3, mmiliki akiwa bwana JEETU Patel ( Jina
halisi Jayantkumar Chandubhai Patel). *
Mheshimiwa Spika, *hii ndio Tanzania ambayo, wazawa wananyang’anywa ardhi,
maeneo yote muhimu na yakimkakati na kukabidhiwa wageni, au watu wenye
mamlaka na fedha, huku ikiwaacha wazawa kubaki vibarua au wakulima wadogo
wanaotegemea hisani ya mabeberu!*
Mheshimiwa Spika, *bado mustakabali wa shamba la mahindi Mbozi
haujajulikana, serikali inataka kumpa mwekezaji, wakati wananchi wana uhaba
wa ardhi kwa matumizi yao! Kambi ya upinzani inaitaka serikali itoe majibu
kuhusiana na hatma ya shamba la mahindi mbozi. Halikadhalika, *Kambi ya
Upinzani inaitaka serikali iliambie Bunge hili tukufu, ni vigezo gani
vilivyotumika kupata wanunuzi wa shamba la Mpunga la Mbarali , shamba la
Kapunga, na mashamba husika yaligawiwa kwa maslahi ya nani?
*
*MKOA WA MARA
*
*Mheshimiwa Spika, *Musoma mjini kumekuwa na mtafaruku mkubwa kati Jeshi la
wananchi JWTZ na wananchi wa Bukanga na Buhare (Mgaranjabo) kutokana na
jeshi kujimilikisha maeneo yao ya asili, waliyokuwa wakitumia kwa ajili ya
matambiko kwa Kabila ya Wakwaya. Hivi sasa wananchi hao hawaruhusiwi kuingia
katika eneo hilo, jambo hilo limezusha chuki kubwa sana kati ya Jeshi na
jamii ya Wakwaya wakazi wa Musoma Mjini.
*MKOA WA MOROGORO*
*Mheshimiwa Spika,*Matatizo ya ardhi,kwa wakubwa kunyang’anya wanyonge ardhi
imeikumba pia Halmashauri ya wilaya ya Mvomero. Mgogoro huu unahusu shamba
namba 299 (iliyokuwa NARCO Ranches),lenye ukubwa wa hekta 49,981. *
Mheshimiwa Spika,* katika shamba hili, taarifa zinaonyesha kwamba 30,007
hektas walipewa Mtibwa sugar licha ya malalamiko kutoka kwa wananchi kwamba
eneo walilopewa ni kubwa sana. Taarifa za kiuchunguzi, zinaonyesha kwamba,
maeneo ambayo yalikuwa yamepangwa kugawiwa wanakijiji, wa kijiji cha Wami,
yamegawiwa ’wananchi’ wafuatao:
1) Bwana Philip Mangula, aliyekuwa katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi, ndio
anaongoza kwa kuwa ’mwanakijiji’ mwenye eneo kubwa, alipewa hekta 2000.
2) Bwana John Malecela, Waziri Mkuu Mstaafu na Makamu Mwenyekiti wa CCM
alipewa hekta 100,
3) Jenerali mstaafu Ngwilizi, ambaye pia alikuwa waziri wa serikali za mitaa
awamu ya tatu alipewa hekta 100 kati ya hekta 5000, zilizosemwa wamepewa
wakulima wadogowadogo wa kijiji.
4) Rais Mstaafu, Ali Hassan Mwinyi, anamiliki hekta 2000, ambazo
hazijaendelezwa,
5) Waziri Mkuu Mstaafu wa awamu ya tatu, Mhe. Frederick Sumaye hekta 500 na
6) Rais wa awamu ya tatu Mhe. Benjamin William Mkapa, hekta 1000 (ila
tofauti na wengine shamba hili limeendelezwa).
*Mheshimiwa Spika, *Kambi ya upinzani inahoji, kama hawa watajwa hapo juu ni
wakazi wa kijiji cha Wami- Dakawa? Na ni vigezo gani vilitumika kuwanyima
ardhi wanakijiji na kuwapa wakubwa hawa? Serikali haioni kwamba mgao huu wa
ardhi uliojaaa dhuluma na upendeleo unahatarisha maisha ya watanzania na
usalama wa nchi kwa ujumla? *
Mheshimiwa Spika*, Wananchi wa maeneo haya wana hasira na serikali yao kwa
kuwa wameshaambiwa hakuna tena eneo la kugawa, wakati walitozwa shilingi
20,000 kila mmoja kwa madai kwamba wangepewa hekta 5. Ahadi ya hekta 10019
kwa wakulima na wafugaji, imegeuka hewa! Tunakwenda wapi kama nchi?
Mheshimiwa Spika Kambi ya upinzani , inaitaka serikali kuangalia upya zoezi
la ugawaji wa ardhi katika maeneo yote yenye utata! Ambayo yalitawaliwa na
rushwa,ubabe na udanganyifu.
*MKOA WA PWANI -SIMBA MOTORS VS WAKAKIJIJI KITONGOJI CHA UNDINDIVU, MAPINGA
– BAGAMOYO*
*Mheshimiwa Spika,* wananchi wa Kijiji cha Mapinga, kitongoji cha Undindivu
chenye idadi ya watu zaidi 1400 wamekuwa wakimiliki eneo la Undindivu kwa
ajili ya kilimo na ufugaji toka mwaka 1960. Kama ilivyo kawaida yetu
,kampuni ya Simba Motors (T) Ltd ilimilikishwa eneo lote la kitongoji cha
undindivu bila wananchi au serikali ya kitongoji na kijiji kujulishwa. Kampuni
hiyo ilipima kwa kutumia mpimaji binafsi na ilimilikishwa shamba hilo lenye
hecta 322. Baada ya kampuni husika kupima na kumilikishwa bila kufuata
sheria, takriban miaka 17 imepita kampuni hiyo haijawahi kuendeleza shamba
hilo,kampuni haijawahi kuliendeleza eneo hilo, si kwa kilimo au ufugaji.
*Mheshimiwa Spika, *mpaka sasa, kuna mgogoro mkubwa baina ya Simba Motors na
wananchi wa kitongoji cha undindivu, na kutokana na shamba husika
kumilikishwa kwa tajiri mmoja , wakati wakazi wa maeneo hayo wamekosa;1) Maeneo
kwa ajili ya huduma muhimu za jamii. 2) Maeneo kwa ajili ya kupanua makazi
yao ya kuishi,kwa sababu robo tatu ya eneo la kijiji limamilikiwa na tajiri
huyo.*
Mheshimiwa Spika,* Kambi ya upinzani inaitaka serikali, kuutafutia mgogoro
huu ufumbuzi wa kudumu. Hatuwezi kuendelea kukaa kimya , na kuacha wananchi
wetu masikini wakipokonywa maeneo yao kwa faida ya matajiri wachache!
Mheshimiwa waziri , Kambi ya upinzani inajua kwamba ofisi yako ilishaletewa
taarifa kwa barua ya tarehe 15/12/2010,hakuna kilichofanyika mpaka sasa.
Tunataka majibu!*
MKOA WA RUKWA – AGRISOIL , KILIMO KWANZA NA HATMA YA TANZANIA*
*Mheshimiwa Spika, *Nchi yetu imefika hapa ilipo, kutokana na watu wenye
dhamana kuingia mikataba mibovu ambayo badala la kuisaidia nchi imekuwa ni
msalaba mkubwa ! na kuwaacha watanzania katika limbwi la umasikini. Hivi
karibuni kampuni ya Agri- Sol Energy LLC na Kampuni ya Serengeti advisors
Ltd , inayoongozwa na Bwana Iddi Simba (aliyekuwa Waziri wa viwanda na
Biashara, awamu ya tatu) na Betram Eyakuze kwa pamoja wameunda kampuni ya
Agrisol Energy Tanzania , wameingia mkataba na Halmashauri ya Wilaya ya
Mpanda. Mkataba ambao unatarajia kuipa kampuni husika miliki ya miaka 99 ya
maeneo ya *lugufu, Hekta 80,317* na *Mishamo hekta 219,800*.*
Mheshimiwa Spika, *Masharti ya Msingi katika makubaliano baina ya
Halmashauri husika na wawekezaji ni yafuatayo;
a) Kodi ya ardhi ( Land rent) ambayo ni Tshs. 200 kwa hekta
b) Ushuru wa kisheria wa Halmashauri ,
c) ada itakayolipwa halmashauri ni Tsh 500 kwa hekta.
d) Na sharti la mwisho, kama mgogoro utatokea baina ya pande zote mbili, *
busara* itatumika kutatua mgogoro, ikishindikana chemba ya Biashara ya
Kimataifa ( ICC) ndio atakuwa msuluhishi! *
Mheshimiwa Spika*, tunakwenda wapi? Umasikini ndio utufanye tuwe mambumbu wa
kufikiri? Hivi kwa nini hatujifunzi ?*
Mheshimiwa Spika,* Katika hatua za awali,madiwani wa Halmashauri husika
walikataa kutoa maeneo yote mawili,waliagiza mwekezaji apewe eneo moja na
kwa kipindi cha miaka 20. Kama ataonekana kufanya vizuri,wangefikiria
kumwongezea muda na eneo! Kama kawaida, walioonekana kuwa wakali wakapelekwa
Marekani, kwa siku nne! Baada ya kurejea, Nchi ikaingizwa kwenye mkataba
mwingine ambao utaigharimu nchi miaka mingine 99 kuweza kujinasua! *
Mheshimiwa Spika, *Si dhamira ya kambi ya upinzani kudhihaki ama kukatisha
tamaa uwekezaji , tunafahamu kwamba serikali inaichukulia Agri Sol Energy
kama sehemu ya mkakati wake wa Kilimo Kwanza, lakini hawa wawekezaji ambao
wanaitwa wakubwa, mashamba ambayo wanayaendesha ,haswa yale yaliyoko
Marekani na yaliyotembelewa na maafisa wa serikali ,wakiongozwa na ofisi ya
Waziri Mkuu yana ukubwa wa ekari 17,900, (ambapo ekari 13,195 ni za mahindi
na ekari 4705 ni maharage). Na shamba hilo limeajiri watu 13, hivi hawa ni
wakulima kweli?
*Mheshimiwa Spika,*Itakumbukwa kwamba kulikuwa na mkakati uliokuwa
ukiendeshwa kwa usiri mkubwa na kwa kasi ya hali ya juu kupitia Ofisi ya
Waziri Mkuu, TAMISEMI wa kuwasambaza wakimbizi wanaokadiriwa kufikia 162,000
nchi nzima, katika mikoa mbali mbali. Mchakato ambao ulipata upinzani mkubwa
hapa Bungeni na kutoka mikoa husika. Huu ulikuwa ni mkakati wa makusudi ili
maeneo husika yawe wazi kwa wawekezaji hao kukabidhiwa, na mbaya zaidi
wakimbizi waliambiwa bayana kwamba sharti la kupewa uraia wa Tanzania ni
kuondoka maeneo hayo!*
Mheshimiwa Spika, *Ni muhimu ikaeleweka kwamba, huu mtindo wa kuwageuzwa
watanzania manamba ndani ya nchi yao kwa kutoa ardhi kwa wageni utakuja
kusababisha machafuko hapo baadae….*ieleweke hoja hapa sio kulisha taifa
na kupata ziada kusafirisha nje ya nchi, hoja hapa ni kumnufaisha mtanzania
katika mipango yote endelevu ya matumizi ya ardhi! Na kama ni suala la
chakula na kusafirisha nje ya nchi chakula hicho kipo tatizo ni kukitoa kwa
wakulima na kufikisha sokoni, ushahidi huo upo kuwa mahindi ni mengi kuliko
uwezo wa wananuni (Rukwa, Songea, Iringa-Ludewa n.k.)
*
*UKIUKWAJI WA SHERIA YA ARDHI, NO. 4 YA MWAKA 1999*
*
Mheshimiwa Spika, *Vifungu vya 19(2) ,20 (1), 20 (2), 20(3) na 20(4) vya
Sheria ya Ardhi vinatoa masharti ya umiliki wa ardhi kwa watu ambao sio
watanzania. *Kwa ujumla wake vifungu husika vinapiga marufuku ardhi kupewa
kwa wageni, isipokuwa tu kwa madhumuni ya uwekezaji chini ya Sheria ya
uwekezaji , No. 26 ya mwaka 1997.* Na ili ardhi husika iweze kupatikana
lazima kwanza itambuliwe ,itangazwe kwenye gazeti la serikali na iwe ‘
allocated’ kwa Kituo Cha Uwekezaji, ambacho ndicho kitakuwa na jukumu la
kumpatia Mwekezaji.*
Mheshimiwa Spika,* Haya yote hayajafanyika, na kinachotaka kufanyika kwa
kutumia vibaraka wa kitanzania , ni kuhakikisha kwamba wabia ‘vibaraka’ wa
kitanzania wana kuwa na hisa nyingi katika umiliki wa ardhi ili kuepuka
kikwazo cha kupitia katika Kituo cha uwekezaji. *
Mheshimiwa Spika*, kuhusu mamlaka ya kuingia ubia (joint venture) na
mwekezaji ambaye si Mtanzania kama ambavyo inaonekana ni kamchezo ambako
kanataka kuchezwa na Serengeti Advisers Limited, Mabadiliko ya Sheria ya
Ardhi yaliyofanyika mwaka 2004, Sheria Na. 2/2004 The Land (Amendment ) Act
2004 Kifungu 19 (1), (2) (c) kinasema ili kufanikisha masharti ya
uendelezaji wa ardhi, *raia wa Tanzania* anayemiliki ardhi anaweza kuingia
‘joint venture’ na mwekezaji ambaye si raia wa Tanzania kwa madhumuni ya
uwekezaji chini ya Sheria ya Uwekezaji , Sura ya 38.
Kwa mujibu wa Kifungu hicho ubia unafanywa na mzawa na mgeni. Kwa mujibu wa
Sheria ya Uraia ‘ The Tanzanian Citizenship Act’, Cap 357. *Shirika la umma
au Kampuni au halmashauri haiwezi kuwa na sifa za kuwa raia. Hivyo kwa
mujibu wa kifungu 19 (2) (c) si halmashauri ya wilaya ya Mpanda wala kampuni
ya Serengeti Advisers yenye uwezo wa kutoa ardhi yake kwa mtu ambaye si raia
ili kuwekeza kwa pamoja.**
Mheshimiwa Spika*, kwa kuzingatia maelezo ya vifungu nilivyovitaja hapo
juu(isipokuwa kama kuna mabadiliko ya sheria ambayo hadi sasa haifahamiki),
Halmashauri ya wilaya ya Mpanda na kampuni ya Serengeti Advisers haina uwezo
wa kuwekeza kwa pamoja ‘ joint venture ‘ *na wawekezaji ambao si watanzania
*mpaka hapo sheria zitakapofanyiwa marekebisho.
Kambi ya upinzani inaitaka Serikali ituambie, ilitumia utaratibu gani wa
kisheria kuingia Mkataba huo wa kifedhuli na usio na maslahi hata kidogo kwa
Halmashauri ya Wilaya ya Mpanda na Taifa kwa ujumla? Nani aliwatuma?
*MIGOGORO YA ARDHI BAINA YA WAKULIMA NA WAFUGAJI*
*Mheshimiwa Spika,* Kilimo na ufugaji ni ya sekta zinazoongoza kwa kutoa
mchango mkubwa sana katika pato la Taifa, halikadhalika ndizo zinazoongoza
kwa kutoa ajira kwani zaidi ya 80% ya Watanzania wamejiajiri katika sekta
hii,haswa vijijini. Hivyo basi kuboresha hizi sekta mbili, maana yake ni
kwamba tutakuwa tumeboresha 80 % ya maisha ya watanzania, kwa kuwa na
uhakika wa kipato, usalama wa chakula na kuongezeka kwa pato la Taifa.*
Mheshimiwa Spika,* Imekuwa ni jambo la kawaida kwa nchi yetu kutokea kwa
migogoro baina ya wakulima na wafugaji, chanzo cha migogoro hiyo ni kutokana
na kutokuwa na mipango thabiti ya serikali ili kubainisha /kutenganisha
maeneo maalum kwa ajili ya wakulima , halikadhalika wafugaji.*
Mheshimiwa Spika, *Sheria yetu ya ardhi , No. 4 na No. 5 ya mwaka 1999
imeainisha utaratibu ambao miliki ya ardhi ya mtu mmoja mmoja ama kikundi
inavyotambulika kisheria mijini na vijijini kisheria ama kimila. Hata hivyo
utaratibu wa utwaaji na umiliki ardhi hasa vijijini kwa matumizi ya wafugaji
, wachungaji na wawindaji haujaainishwa ipasavyo !Mikakati ya kutenga ardhi
hasa ya wafugaji imekuwa finyu mno kiasi kwamba wakulima na wawekezaji
wameendelea kuhodhi/kuvamia ardhi ya wafugaji kwa msaada wa mawakala wa
serikali.[6]
wamekuwa wakivamia maeneo ya wakulima kutokana na kukosa maeneo mwafaka kwa
ajili ya malisho.
*Mheshimiwa Spika,*Tafiti pia zimeonyesha kwamba ardhi ya wafugaji imekuwa
ikichukuliwa kwa ajili ya matumizi ya wawekezaji , kugeuzwa kuwa hifadhi za
taifa au game reserves! Matokeo yake wafugaji wanageuka watu wa
kutangatanga! Wakati serikali imekuwa ikiwataka wafugaji waondokane na njia
za kizamani za kufuga, bado haijaonyesha njia mbadala za ufugaji wa kisasa!*
Mheshimiwa Spika, *Kambi ya upinzani inaitaka serikali , itueleze ina
mikakati gani katika kuhakikisha kwamba maeneo rasmi ya wafugaji
yanabainishwa ili kuepusha umwagaji damu na migogoro isiyo na tiba huko
mbeleni.
Halikadhalika, kambi ya upinzani inaitaka serikali itoe tamko juu ya tatizo
la mpaka na mgogoro wa wakulima na wafugaji wa jamii ya Wamasai katika eneo
la *vijiji vya Izava (Chamwino) na Chitego (Kongwa).* Mgogoro ambao kwa
kiasi kikubwa ulisababishwa na maamuzi ya kibabe yaliyofanywa na wakuu wa
wilaya hizi mbili (mwaka 2006) , wakishirikiana na Mwenyekiti wa Halmashauri
kipindi hicho!*
Mheshimiwa Spika*, Wakulima wa maeno haya wanalalamikia wafugaji ambao
waliingizwa kibabe katika maeneo yao, bila kuwashirikisha kwa nguvu za ’*kigogo
mmoja*’, matokeo yake mashamba yao ndio yamegeuka malisho ya mifugo hiyo!
Kumekuwa na tuhuma ya ushiriki wa skari wa Kongwa katika zoezi hili
kandamizi! Kambi ya upinzani inaitaka Serikali ifuatilie mgogoro huu ili
kuepusha maafa yanayoweza kutokea, hasa ikizingatiwa kwamba matukio ya
kushambuliana ,kujeruhi na kutishia maisha imekuwa ni jambo la kawaida baina
ya pande mbili.*
MATATIZO YA TATHMINI NA MALIPO YA FIDIA*
*Mheshimiwa Spika, i*mekuwa ni jambo la kawaida kwa wananchi kulalamika
kupunjwa ama kutokulipwa kabisa fidia pale ambapo wanatakiwa na serikali
kuhama maeneo yao ili kupisha matumizi mapya ya ardhi. Mheshimiwa Spika
sheria zetu zinatamka bayana kwamba, pale ambapo mwananchi anapochukuliwa
eneo lake na serikali kwa mamtumizi mengine na hivyo kutakiwa kuhama
anatakiwa kulipwa fidia inayojumuisha, thamani ya ardhi, usumbufu, usafiri
na hasara ambayo muathirika ataipata kutokana na kuchukuliwa eneo lake. *
Mheshimiwa Spika, *hata hivyo kumekuwa na malalamiko kila pahala ambapo
wananchi wanatakiwa wasimamishe shughuli zao kupisha matumizi mapya ya
ardhi. Serikali hailipi fidia ya kutosha na hata wananchi wakilalamika
serikali inaendelea miradi. Badala ya fidia kumwacha mwananchi awe katika
hali aliyokuwa mwanzo,mfumo wa fidia wa nchi yetu ,haswa maeneo
yanapochukuliwa na serikali (ambayo ndio hiyo hiyo inafanya tathmini na
kuamua kiasi gani kilipwe) unamwacha mwathirika fukara zaidi!
a) Kambi ya upinzani inaitaka serikali itoe maelezo juu ya hatma ya wananchi
wa Kurasini Mabwawani ambao tangu nyumba zao zifanyiwe tathmini miaka miwili
iliyopita ili kupisha upanuzi wa bandari, kumekuwa na kimya kingi na
wakiuliza kuhusu hatma yao, hawajibiwi kitu!kuna kundi ambalo limelipwa,
kuna kundi lingine halielewe nini kinachoendelea na wanashindwa kuendeleza
maeneo yao
b) Kambi ya upinzani inaitaka wizara ya ardhi itoe maelezo juu ya hatma ya
wananchi wa kijiji cha Mabwepande, kata ya Mabwepande Jimbo la Kawe ambao
miaka minne iliyopita serikali ilikwenda kufanya tahmini na kuwaagiza
wananchi kutokufanya maendeleo yoyote ili kupisha upanuzi wa chuo cha IFM.
Hakuna kilichofanyika mpaka sasa, wananchi waliokuwa wanategemea kilimo,
wamezidi kufukarishwa, serikali ikiulizwa haina majibu. Matokeo yake maeneo
ambayo waliambiwa wayaache sasa yamevamiwa na genge la wavamizi, si wizara,
halmashauri ya manispaa ya kinondoni ama vyombo vya usalama vinavyochukua
hatua licha ya kupewa taarifa ya uvamizi huu!
c) Kambi ya Upinzani inaitaka serikali ieleze hatma ya wananchi wa Kigamboni
(ambao wengi walikuwa wanafanya kazi za kilimo) ambao wanalalamikia zoezi la
kuchukua maeneo yao kupisha ujenzi wa mji mpya wa Kigamboni kutawaliwa na
rushwa, maeneo kuthaminishwa bei ndogo, wakati huo huo serikali baada ya
kulipa fidia kiduchu wanauza maeneo husika kwa bei ya kutupwa,bei ambayo
mwananchi wa kawaida hawezi kuimudu!*
d) *Kambi ya upinzani inaitaka serikali ieleze hatma ya wananchi wapatao *
1600* wa wilaya ya Mbarali waliotakiwa waondoke maeneo yao ili *kupisha
upanuzi mbuga ya Taifa ya Ruaha?* Serikali ilitoa shilingi bilioni 6.5 tu
kwa wakazi wote. Kwa tathmini ya kawaida kila mwananchi alipewa shilingi
milioni 4.5. *Hivi kwa maisha ya sasa kuna nyumba inayoweza kujengwa na
kukamilika kwa kiasi hicho cha fedha? Huu ni unyonyaji na udhalimu ulio
dhahiri.*
*e) *Kambi ya Upinzani inaitaka serikali ieleze hatma ya fidia ya wananchi
wa Jimbo la Ubungo Kata ya Kwembe wanaopaswa kuhama kupitisha ujenzi wa
majengo wa Chuo Kikuu cha Sayansi ya Tiba ya Afya (MUHAS) Mloganzila. Wakati
wa kuhitimishwa kwa bajeti ya Waziri Mkuu katika mkutano huu wa bunge
serikali ilieza kwamba tathmini ya fidia inaendelea na kwamba wapo wananchi
ambao tayari wamelipwa fidia na wengine bado hawajalipwa mpaka sasa. Kambi
ya Upinzani inaitaka serikali kuzingatia kwamba fidia iliyolipwa kwa
wananchi wachache ni ya mali na mazao; hata hivyo wananchi hawajalipwa fidia
ya ardhi. Ofisi ya Waziri Mkuu ilitoa maelekezo kwa wizara zinazohusika
kuhakikisha fidia stahiki inalipwa. Mwaka 2010 Wizara ya Ardhi na Maendeleo
ya Makazi ilifanya mkutano na wananchi na kuwaahidi kulipa fidia ya ardhi
kwa mujibu wa sheria; kambi ya upinzani inataka serikali ieleze malipo hayo
yatatoka kwenye fungu lipi na yatalipwa lini?*
MALALAMIKO DHIDI YA MAMLAKA YA USTAWISHAJI MAKAO MAKUU (CDA)*
*Mheshimiwa Spika,* Mwaka 2004 , Serikali kupitia wakala wa majengo mkoani
Dodoma, waliwauzia wananchi, nyumba zilizokuwa zinamilikiwa na lililokuwa
Shirika la Reli Tanzania (TRC). Malalamiko makubwa kutoka kwa wananchi hawa
wa Tambukareli,ni kunyimwa hati za nyumba zao na CDA ilhali wameshalipia
nyumba hizo kwa ukamilifu. Sababu zinazotolewa na CDA, zisizo na mashiko ni
kwamba eti Serikali ilitoa uamuzi wa kuuza nyumba bila kuwahusisha CDA ,
hivyo hawatambui uuzwaji wa nyumba hizo!*
Mheshimiwa Spika,*Kambi ya upinzani inaitaka serikali kutoa maelekezo kwa
CDA kutoa hati husika, ni suala la kibri na jeuri kwa taasisi ya serikali
kuhoji maamuzi ya serikali, au leo tuelezwe kwamba Serikali ya Jamhuri ya
Muungano inafanya kazi chini ya CDA? Kama kulikuwa na uzembe ndani ya
Serikali kwa nini Wananchi hawa masikini waliodunduliza vihela vyao wapate
makazi waumizwe? Kambi ya upinzani inataka kauli thabiti ya serikali
kuhusiana na hili!
*
SHERIA NA. 5 YA ARDHI YA VIJIJI NA MUSTAKABALI WA TAIFA*
*Mheshimiwa Spika,*Sheria ya Ardhi ya Kijiji inatoa mamlaka kwa Halmashauri
ya kijiji kusimamia ardhi yote ya kijiji. Halikadhalika Halmashauri ya
kijiji imepewa mamlaka ya kugawa ardhi baada ya kuruhusiwa na Mkutano Mkuu
wa Kijiji. Uzoefu umeonyesha kwamba kutokana na kutokuwa na ufahamu mpana wa
sheria, watu wenye fedha wamekuwa wakitumia fursa hii ya kisheria vibaya kwa
kuwarubuni viongozi wa vijiji, na hatimaye kugawa maeneo ya kijiji kwa
wageni wenye fedha wachache, huku ikiwaacha wanakijiji bila ardhi yoyote. *
Mheshimiwa Spika,*Hali inakuwa mbaya zaidi pale ambapo watu ambao sio
watanzania wanatumia upenyo huu wa kisheria, na kumilikishwa maeneo makubwa
ya kijiji kinyemela! Kambi ya upinzani imepata malalamiko kutoka kwa
wanakijiji wa kijiji cha Orngadida, Kata ya Qash, Babati ( taarifa ambayo
Waziri wa Ardhi, Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Mkuu wa wilaya na Mkurugenzi
Mtendaji –Halmashauri wanayo). Wanakijiji hao wanawatuhumu viongozi wa
serikali ya kijiji wakishirikiana na diwani kuuza Ardhi kwa wageni pasipo
kuwashirikisha, wanakijiji wamemwandikia Mkuu wa wilaya ya Babati barua
mbili ambazo nazo hazijajibiwa! *
Mheshimiwa Spika,* Hakuna ubishi kwamba kuna wageni wengi waliopata maeneo
ya vijiji kinyemela kwa kutumia upenyo huo, wakati sheria ya Ardhi No.4 ,
kifungu na 20 kinakataza wageni kumiliki ardhi nchini isipokuwa kwa malengo
ya uwekezaji tu, na ambao umiliki wake lazima upitie Kituo cha uwekezaji
Tanzania , na si vinginevyo. *
Mheshimiwa Spika,* Kambi ya upinzani inaitaka serikali iliambie Bunge lako
tukufu,ni lini imefanya tathmini katika vijiji vyetu ili kuweza kubainisha
ardhi zilizotolewa na Halmashauri za kijiji na uhalali wake. Ni maoni ya
Kambi ya upinzani kwamba sheria hii isipoangaliwa kwa umakini itasababisha
umwagaji damu mkubwa hasa pale wananchi watakapohisi kunyang’anywa ardhi yao
kifisadi au vinginevyo. Na mbaya zaidi Mheshimiwa Spika,zoezi hili
linafanywa hata mijini, na serikali za mitaa ambazo hazina mamlaka ya kugawa
ardhi. Mchezo ambao wanafanya kwa kushirikiana na watendaji wa manispaa, na
baadhi ya maafisa wa Wizara!
*UVAMIZI WA MAENEO YA WAZI MKOA WA DAR ES SALAAM*
*Mheshimiwa Spika; *kutokana na malalamiko ya wananchi mbalimbali kuhusu
uvamimizi wa maeneo ya wazi ya umma katika mkoa wa Dar es salaam, Serikali
iliunda kamati ya kufanya uchunguzi kuhusu uvamizi katika maeneo husika.
Kamati ilikamilisha kazi yake tarehe 13 Julai 2010. Pamoja na majibu ya
Waziri wa Ardhi na maendeleo ya makazi aliyoyatoa tarehe 1 Julai 2011 wakati
akijibu maswali bungeni kuhusu hatua ambazo serikali imechukua toka mamlaka
husika zilipokabidhiwa ripoti husika; kambi ya upinzani inataka maelezo
zaidi kutoka kwa serikali kwa kuwa mwaka mmoja umepita toka uchunguzi huo
ufanyike na sehemu kubwa ya viwanja bado vipo mikononi mwa wavamizi.*
Mheshimiwa Spika;* kambi ya upinzani inaitaka serikali ieleze: Ni viwanja
vingapi vimerudishwa na vingapi bado vipo mikononi mwa wavamizi? Ni lini
serikali itarejesha viwanja vyote vilivyobaki kwenye matumizi yake kwa
mujibu wa sheria kwa kurejea mapendekezo ya kamati? Ni hatua gani
zimechukuliwa kwa wahusika Wizarani na kwenye halmashauri walioshiriki
kusababisha hali hiyo ukiondoa maafisa wachache ambao wamefikishwa
mahakamani kutokana na kesi ya kiwanja kimoja hivi karibuni? Kwa kuwa sasa
Wizara ina kada ya askari (land rangers) ni lini askari hao watatembelea
maeneo yote yaliyotajwa kuvamiwa kwa mujibu wa taarifa ya kamati ili hatua
stahiki ziweze kuchukuliwa?
*Mheshimiwa Spika;* athari za uvamizi wa viwanja vya wazi ni kubwa katika
mipango miji na maendeleo ya wananchi kwa ujumla. Mathalani katika Manispaa
ya Kinondoni kwenye kiwanja na. 856 Msasani beach ambacho kwa mujibu wa
Ramani ya upimaji iliyosajiliwa namba 29331 ilikuwa ni kwa matumzi ya wazi,
lakini baadae kilimilikishwa kwa mtu binafsi. Athari yake ni kuzibwa kwa
njia ya mkondo kuelekea baharini yamezibwa na hivyo kuleta mafuriko katika
barabara na makazi ya watu wa eneo husika; hali hiyo ipo pia katika majengo
ya May Fair na Markham. Kambi ya Upinzani inataka Serikali ieleze hatua zipi
itachukua ili kuepusha wananchi wa maeneo ya Msasani, Mikocheni na maeneo
mengine katika jiji la Dar es salaam yaliyojengwa majengo kinyume cha sheria
na mipango miji na hivyo kuleta athari kubwa kwa maisha ya wananchi.*
SEKTA YA NYUMBA**
Mheshimiwa Spika,* sekta hii ni sekta pekee inayoweza kuleta na kutekelezwa
kwa dhana nzima ya maisha bora kwa kila mtanzania. Nchi yetu na watanzania
kwa ujumla bado tuna matatizo makubwa ya nyumba bora na za bei nafuu
kutokana na bei kubwa ya cement na bati bidhaa muhimu katika kutimiza azma
ya ujenzi.
*Mheshimiwa Spika,* tulisema na tunasema kuwa bei ya simenti na bati inaweza
kuwa chini ya shilingi elfu saba, kama serikali itakuwa na utashi wa
kuwahudumia wananchi kwa dhati, Wakati ukinunua simenti Uturuki, na
Paksitani ukinunua tani 600,000 bei ya tani moja ni dola za Marekani 70 hadi
bandarini. Guangzhou –China tani moja ni dola za marekani 26. Kwa hesabu za
kawaida kwa mfuko mmoja ni dola 3.5 sawa na shilingi 5,250 kama ukinunua
Pakstani au Uturuki, Ukinunua China bei itakuwa dola 1.3. *
Mheshimiwa Spika*, Kambi bado inasisitiza kuwa kama Serikali inadhamira ya
kweli mfuko wa simenti hauwezi kuuzwa zaidi ya shilingi 7,500. Hivyo basi
tunaitaka Serikali itueleze kwanini bei ya simenti inauzwa zaidi ya shilingi
14000 kwa Dar es salaam na kwa nje ya Dar es Salaam bei ni zaidi ya hapo,
wakati malighafi zinapatikana hapa hapa nchini na kiwanda kikubwa cha
simenti kinatumia gesi asili ili kupunguza gharama za umeme. *
Mheshimiwa Spika,* Serikali ina mkakati gani wa kupunguza gharama hizi na ni
faida kiasi katika kodi tunayopata kwa kuwalangua watanzania. Serikali
haioni kwamba ina wajibu wa kuondoa hizi kero wananchi wajenge nyumba bora
na kwa bei nafuu?
*SHIRIKA LA NYUMBA LA TAIFA-(NHC)*
*
Mheshimiwa Spika,*Shirika la Nyumba la Taifa, lilipoanzishwa mwaka 1962 ,
moja kati malengo yake ilikuwa ni kujenga nyumba za bei nafuu kwa ajili ya
watanzania wafanyao kazi mijini . Hata hivyo kwa kadiri siku zilivyosonga
mbele, shirika hili liligeuka kutoka kuwahudumia masikini na watu wenye
kipato cha kati na badala yake kuwahudumia watu wa kipato cha juu. *
Mheshimiwa Spika*, Shirika la Nyumba la Taifa linahudumia asilimia 0.5 tu ya
watanzania wote wa nchi hii, swali la msingi ni je Serikali imeweka mikakati
gani ya kuhakikisha kuwa shirika hili linahudumia watanzania wengi zaidi kwa
kuwapatia nyumba za bei nafuu.*
Mheshimiwa Spika,*Kama ilivyoripotiwa na vyombo vya habari, mwezi Juni 2010,
Katibu Mkuu wa wizara ya ardhi, akikerwa na hali ilivyokuwa katika Shirika
la Nyumba, alisema kwa sasa NHC ndilo shirika la umma linaloongozwa kwa
rushwa nchini Tanzania, na kwamba *baadhi* ya watumishi waandamizi
wameligeuza shirika hilo kuwa ni ng’ombe wao wa kukamua fedha
chafu!.[7]
mbele zaidi, kwa kutolea mfano wa nyumba iitwayo
Victoria house iliyopo kando ya Barabara ya Ali hassan Mwinyi ambayo pesa ya
pango ilikuwa ikiingia kwenye akaunti ya mtumishi wa shirika*.**
Mheshimiwa Spika, *kumekuwa na malalamiko pia ya kutokuwa na uaminifu baina
ya wapangaji, wakishirikiana na washirika wao walioko kwenye utumishi wa
shirika, kulikopelekea shirika kupata hasara ya mabilioni ya shilingi kwa
kuingia mikataba tata! Kwa mujibu wa vyanzo vya taarifa hizi, mikataba tata
imekuwa ikifanyika huku ikiwashirikisha wapangaji wa asili ya kihindi kwa
kiasi kikubwa ambao wanatuhumiwa kuligeuza shirika hilo kama mali yao
binafsi. *
Mheshimiwa Spika, *mwaka mmoja ukiwa umepita tangu kauli hii nzito toka kwa
mtendaji wa ngazi ya juu wa wizara,Kambi ya Upinzani inaitaka serikali
ilieleze Bunge hili tukufu , ni hatua gani zimechukuliwa dhidi ya watumishi
hawa , na ni hatua gani zimechukuliwa dhidi ya wapangaji wasio waaminifu!*
SERIKALI NA TAASISI ZAKE KUTOLIPA KODI ZA PANGO KWA WAKATI*
*
Mheshimiwa Spika,*Katika kipindi cha julai 2011 shirika lilikusanya kodi za
pango pamoja na malimbikizo kiasi cha shilingi bilioni 31.
Pamoja na na jitihada za kukusanya kodi na malimbikizo na hasa yale
yanayodaiwa serikali na taasisi zake, malimbikizo bado ni makubwa . Hadi
machi 2011, serikali na taasisi zake ilikuwa ikidaiwa kiasi cha shilingi
bilioni 1.543, baada ya kupunguza malimbikizo kwa kiasi cha shilingi milioni
115, sawa na asilimia 8 tu!Kambi ya *upinzani* inataka serikali ieleze ni
kwa nini imekuwa ni mdaiwa sugu, na kwa nini hailipi madeni ya shirika la
nyumba?
*MIKOPO YA UNUNUZI NA UJENZI WA NYUMBA**
Mheshimiwa Spika,* Pamoja na kuwepo kwa sheria ya Mikopo ya nyumba (mortgage
financing act) ya mwaka 2008 na sheria ya umiliki wa sehemu ya majengo (
unit titles act) ya mwaka 2008, masharti ya mikopo hii bado ni magumu.
Mfano, kwa sasa benki zanazotoa mikopo ya nyumba masharti yake ni pamoja na
muda wa marejesho ya kati ya miaka 6 mpaka 15 na riba kati ya asilimia 17
mpaka 22 kwa mwaka .
*Mheshimiwa Spika, *Iwapo hali hii haitabadilika , itakuwa vigumu kwa
wananchi, halikadhalika shirika letu la nyumba kujenga nyumba za gharama
nafuu na kwa wananchi walio wengi kuweza kumudu mikopo ya ununuzi wa nyumba.
*
Kambi ya upinzani,* inaitaka Serikali itueleze ni kwa namna gani imejipanga
kuweza kutatua tatizo hili ! Lazima Serikali iweke Mazingira ya kuziwezesha
Benki kutoa mikopo yenye masharti nafuu kwa wawekezaji na wanunuzi wa
nyumba.!!!!
*
KODI YA ONGEZEKO LA THAMANI (VAT) NA ONGEZEKO LA MTAJI (CAPITAL GAIN TAX)
KWENYE MAUZO YA NYUMBA ZINAZOJENGWA NA SHIRIKA*
*Mheshimiwa Spika, *changamoto kubwa inyowakabili watanzania wengi ni kuweza
kupata nyumba za bei nafuu. Kwa sheria zetu za kodi, nyumba mpya iliyojengwa
kwa ajili ya kuuzwa inapaswa kutozwa kodi ya ongezeko la thamani (VAT) pale
inapouzwa, na anayelipa kodi hiyo ni mnunuzi!
*Mheshimiwa Spika,* suala la msingi ni kuwa nyumba hiyo wakati inajengwa
vifaa vyote vya ujenzi ulipiwa kodi hiyo, hivyo kitendo cha mnunuzi kulipa
kodi ya VAT wakati wa kununua nyumba hiyo ni kulipia kodi mara mbili (DOUBLE
TAXATION). Je, serikali haioni kama haimsaidii mwananchi kuweza kuishi
kwenye nyumba nzuri na kwa gharama iliyonafuu?
*Kambi ya Upinzani* inaitaka Serikali kuangalia upya mkakati wake wa
kuwanyang’anya watanzania hata kile kidogo walichonacho badala ya
kuwaongezea umasikini iwe ni kuwapa maisha bora kama kauli mbiu yenu
inavyosema. Mfano dhahiri, kwa mwaka wa fedha 2010/11 shirika lilitarajia
kujenga *nyumba 49* , zenye jumla ya thamani ya shilingi *bilioni 4.08.* Kwa
gharama iliyotumika, wastani wa nyumba moja ililigharimu shirika
shilingi *milioni
83.4**.
**Mheshimiwa Spika, *kwa mujibu wa Taarifa ya utekelezaji wa Kazi za Shirika
la Nyumba la Taifa kuanzia Julai 2010 hadi Mei 2011 wanatarajia kupata
shilingi *bilioni 6.3 *kutokana na mauzo ya nyumba hizo , yaani faida ya
shilingi *bilioni* *1.9 *Kwa tafsiri nyingine nyumba moja itauzwa na shirika
la nyumba kwa shilingi milioni *129.2*, wakati gharama halisi za ujenzi ni
shilingi *milioni 83.* Kwa kila nyumba iliyounzwa shirika limepata faida ya
shilingi *milioni 46.**
MUSTAKABALI WA NYUMBA ZA SHIRIKA LA NYUMBA**
Mheshimiwa Spika,* Hivi karibuni kumekuwa na sintofahamu nyingi kuhusiana na
nyumba za shirika. Wapangaji (hususan katika maeneo ya katikati ya miji)
wamekuwa wakilitaka shirika liwauzie nyumba. Kambi ya upinzani inaitaka
serikali itoe kauli, nini msimamo wake kuhusiana na suala
hili,[8]
hakuna haja yeyote ya shirika hili kuuza nyumba
hizo na badala yake iweke mkazo katika kujenga nyumba ambazo zitapangishwa
kwa bei nafuu.*
Mheshimiwa Spika, *Sheria ya mikopo yaani *”**Government Loans, Guarantees
and Grants Act 1974 and amendments 2003″ *inalifanya shirika la nyumba la
taifa kulazimika kupata kibali kutoka Wizara ya Fedha hata pale ambapo
halihitaji kupata dhamana ya serikali na pia hata kwa mikopo ya ndani ya
nchi. Wote tunafahamu rasilimali ambazo shirika hili linazo. Pamoja na
kufahamu yote, bado tumeamua kuliweka shirika hili katika urasimu mkubwa wa
kiserikali wa kupata vibali kutoka wizara ya fedha bila ya sababu za lazima.
Je, serikali imedhamiria ya kutekeleza ahadi zake katika ujenzi wa nyumba na
kuliwezesha shirika kujiendesha kibiashara kama sheria yake inavyolitaka?
Kambi ya Upinzani inaitaka serikali itoe ufafanuzi ni lini inatarajia
kuanzisha mchakato wa kurekebisha sheria hiyo?
*MPANGO WA UENDELEZAJI ENEO LA KIGAMBONI*
*Mheshimiwa Spika,* tangu mwaka 2007, Wizara ilianza hatua za awali za
kuendeleza mji mpya wa Kigamboni. Mradi huu unahusisha hekta 6500
linaloshirikisha kata 5 za Kigamboni, Tungi,Mjimwema,Vijibweni, Kibada na
mitaa miwili ya Mbwamaji na Kizani kwenye Kata ya Somangila.*
Mheshimiwa Spika, *Miaka minne imepita,Kambi ya upinzani inaitaka serikali
ibainishe ni lini hasa mradi huu utaanza, na michakato ya fidia kwa wananchi
imefikia wapi,na ni utaratibu upi unaotumika kulipa fidia husika.
Halikadhalika Kambi ya upinzani inaitaka serikali kuhakikisha kwamba
kunakuwepo kwa utaratibu ulio wa uwazi, pasi na upendeleo kuhakikisha kwamba
wananchi waishio ndani ya eneo la mpango ( yaani wakazi wa kata zote tano)
wanabaki kwenye eneo hilo, kama ambavyo madhumuni ya mpango unavyoainisha. *
Mheshimiwa Spika,*Kambi ya upinzani ina taarifa juu ya mchakato unaofanyika
baina ya serikali na shirika la nyumba la taifa unaohusiana na uendelezaji
wa eneo la *Tanganyika Pakers-Kawe*, kama ilivyobainishwa na naibu waziri wa
viwanda na biashara, wakati akijibu swali namba *246*, ambapo pamoja na
mambo mengine alikiri kwamba katika eneo la kawe kuna heka 180, ambalo ni
eneo la makazi na ambalo halikuuzwa na Serikali kwa mwekezaji.Kambi ya
upinzani inaitaka serikali ifahamu kwamba , eneo husika bado lina wakazi
ambao walikuwa ni wafanyakazi wa Kiwanda cha Tanganyika Pakers, na hatua
zozote za kuliendeleza eneo husika,lazima uhakikishe unawahusisha kikamilifu
wananchi hao! Ambao wameishi eneo hilo maisha yao yote. *
MAMLAKA YA/WAKALA WA KURATIBU BEI ZA PANGO LA NYUMBA*
*Mheshimiwa Spika, *kutokana na ongezeko kubwa la watu mijini, mahitaji ya
nyumba za kupanga yamekuwa ni makubwa sana . Imekuwa ni jambo ka kawaida kwa
wenye nyumba kujipangia bei za kodi ya nyumba kwa kadiri wanavyoona inafaa
wao, kwa kuwa hakuna chombo cha kuwathibiti. Matokeo yake kodi ya nyumba
imegeuka mzigo mkubwa sana kwa wananchi wa kawaida. Kambi ya upinzani
inaitaka serikali, iweke utaratibu utakaotambulika kisheria utakaoweka
mwongozo na kuweza kuwadhibiti gharama za kodi za nyumba kwa ujumla wake.
Kwa maana nyingine ni kuanzisha mamlaka ya udhibiti itakayoitwa *”Real
Estate Regulatory Authority”.*
*
WAKALA WA TAIFA WA UTAFITI WA NYUMBA BORA NA VIFAA VYA UJENZI- (NHBRA)*
*Mheshimiwa Spika, **Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba Bora na Vifaa vya
Ujenzi (NHBRA)*, jukumu la Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba Bora na
Vifaa vya Ujenzi (National Housing and Building Research Agency – NHBRA) ni
kufanya tafiti, kuelimisha, kukuza, kushauri, kuhamasisha na kusambaza
matokeo ya utafiti na utaalam wa ujenzi wa nyumba bora na za gharama nafuu.
Lengo la Wakala ni kuinua na kuboresha viwango vya nyumba kwa kutumia vifaa
vilivyotafitiwa na vipatikanavyo hapa hapa nchini jambo ambalo litaongeza
ubora wa maisha ya wananchi mijini na vijijini ili kutimiza malengo ya
MKUKUTA. *
Mheshimiwa Spika,* kambi ya upinzani inataka ipewe taarifa ni kwa namna na
kiasi gani wakala huu umefanikiwa kutimiza malengo ya kuanzishwa kwake kwani
ujenzi wa nyumba za matope, fito na nyasi bado uko pale pale jambo ambalo
linasababisha maisha bora kwa kila mtanzania kuwa ni kitendawili kwa miaka
mingi ijayo!*
MUHSTASARI WA MATUMIZI YA FEDHA ZA KAWAIDA NA MAENDELEO KWA MWAKA WA FEDHA
2010/2011*
*
Mheshimiwa Spika,*Katika mwaka wa fedha 2010/11 , Wizara iliidhinishiwa
jumla ya shilingi bilioni *53,848,061,000*. Kati ya fedha hizo shilingi *
6,423,295,000* zilitengwa kwa ajili ya mishahara, shilingi
*25,159,688,000*kwa ajili ya matumizi mengineyo na shilingi
*22,265,078,000* kwa ajili ya miradi ya maendeleo. *
Mheshimiwa Spika, *Hadi Mei , 2011 Wizara ilipokea jumla ya shilingi *
27,787,178,679* *(Bilioni 27.7)*sawa na asilimia 51.5 ya tengeo la bajeti
kwa mwaka. Kati ya fedha hizo, shilingi *25,658,017,495* sawa na asilimia
92.5 ya fedha zilizopokelewa , shilingi 13,226,897,075 zilitumika kwa ajili
ya matumizi mengineyo, shilingi 8,499,539,334 zilitumika kulipa mishahara na
shilingi *3,931,581,086* *zilitumika kutekeleza miradi ya maendeleo.*Kambi
ya upinzani inaitaka serikali itueleze ni kwa sababu gani kati fedha za
maendeleo zilizotengwa *( Tshs.22,265,078,000),* zilizoweza kutumika ni
Tshs. *Bilioni 3.9* tu? Ni miradi mingapi iliyokuwa itekelezwe katika mwaka
wa fedha 2010/2011 imeshindwa kutekelezwa kutokana na kukosekana huko kwa
fedha?
*POSHO NA MARUPURUPU VS FEDHA ZA MIRADI YA MAENDELEO*
*Mheshimiwa Spika, *Kambi ya Upinzani tulikuja na hoja ya kuitaka serikali
iangalie upya mfumo wake wa ulipaji posho na marupurupu , lengo likiwa na
kuisaidia serikali kuokoa matumizi yasiyo ya lazima na hatimaye fedha ambazo
tunazitumia kulipana posho tuzielekeze kwenye matumizi yenye tija kwa
wananchi. Tunashukuru kwamba hatimaye tulichokuwa tukikipigia kelele na
kubezwa, kimeanza kutekelezwa na Serikali hii hii . Mhe. Waziri Mkuu wakati
akiliomba Bunge kuahirisha hoja ya Wizara ya Nishati na Madini ili waende
kujipanga upya alitamka yafuatayo , naomba kunukuu:*“Mheshimiwa
Spika,ushauri mlioutoa ni wa msingi sana. Moja mmesema Serikali nunueni
mtambo na tusitafute visingizio vya fedha . Kwamba tafuteni kila mbinu
huko,tafuteni,kateni posho zenu,kateni vitu gani,nendeni mkatazame magari
mnayotumia haya, punguza huko. Tazameni OC yenu kikamilifu,mtaona kule ndani
yako matumizi mengine ambayo mkiamua kwa dhati mnaweza kabisa mkayaondoa
huko, yakaenda yakanunua mitambo ya uhakika,yakawasaidia hata kuongeza uwezo
wa mafuta kwa ajili ya mitambo inayotumia mafuta” Mwisho wa kunukuu.**
Mheshimiwa Spika,*Kumbe inawezekana!Tukiamua kupunguza anasa na starehe na
kuwekeza kwa wananchi wetu,inawezekana! Hakika Inawezekana!Katika Wizara hii
*zaidi ya shilingi bilioni moja*, zimetengwa kwa ajili ya posho(wakati ni
bilioni 3.9 tu zilitumika kwa shughuli za maendeleo). Cha kusikitisha zaidi
hadi karne hii,kuna posho zinatengwa kwa ajili ya kuwalipia baadhi ya
maafisa bili za maji na umeme *‘kwa maofisa wanaostahili’*. Mfumo huu
umesambaa mpaka kwenye Halmashauri zetu.
*Mheshimiwa Spika,* ni wajibu wa serikali kuagalia upya mfumo huu wa
kimwinyi, na kuacha huduma hizi ‘BINAFSI’ zigharamiwe kwa viongozi wa
waandamizi (wakuu) tu, wa mihimili mitatu ya dola! Tatizo kubwa
linalotukumba kama nchi, ni kuendesha mambo kwa mazoea. Lazima
tubadilike! Mheshimiwa
Spika, baada ya kusema hayo, kwa niaba ya Kambi ya Upinzani, naomba
kuwasilisha.
*………………………………………….. ……**
Halima James Mdee(Mb)**
Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani-Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya
Makazi**
15.08.2011*
__,_._,___